Home Mchanganyiko WAZIRI KWANDIKWA AFURAHISHWA NA SKIMU YA UMWANGILIAJI YA CHITA JKT

WAZIRI KWANDIKWA AFURAHISHWA NA SKIMU YA UMWANGILIAJI YA CHITA JKT

0

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena,akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa ambaye alifanya ziara katika kikosi
cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akikagua miundombinu iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akipata maelezo ya  Mhandisi Msimamizi Mkuu wa ujenzi wa Skimu ya umwangiliaji Chita JKT kutoka Wizara ya kilimo Tume ya Taifa ya umwangiliaji Mhandisi Elibariki Mwendo wakati akikagua  miundombinu iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akitoa maelezo wakati akikagua mbegu za Mpunga zilizopo katika shamba la Mpunga  katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akimsikiliza Mtafiti wa kilimo kutoka TARI Dakawa Bw.Barnabas Sitta wakati akikagua mbegu za Mpunga katika Shamba la Mpunga lililopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akiangalia  mbegu za Mpunga katika Shamba la Mpunga lililopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akipata maelezo ya ramani ya mchoro wa Ghala kutoka kwa Mhandisi Majengo JKT Chita ambaye ni Msimamizi wa Ghala  Private Masanja Gonzi  wakati  akikagua  miundombinu iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,,akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele,wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Ujenzi wa Ghala ukiendelea katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT ambapo likikamilika lina uwezo wa kuhifadhi tani 1500 za mazao.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akikagua miundombinu ya Mto Lendi uliopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akiangalia Shamba la Samaki wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Samaki kutoka Kikosi cha 837 KJ Chita Luteni Joseph Lyakurwa, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Muonekano wa Shamba la Samaki lililopo katika kikosi cha 837 Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akicheza na Kikundi cha Sanaa 837KJ mara baada ya  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele,akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,akizungumza na Maafisa ,Askari,Vijana na watumishi wa Umma mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

Baadhi ya Maafisa ,Askari,Vijana na watumishi wa Umma wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe.Elias Kwandikwa,(hayupo pichani) wakati akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji iliyopo katika kikosi cha  837 KJ Chita JKT.

………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Chita,Kilombero

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe. Elias Kwandikwa, amefurahishwa na skimu ya umwagiliaji ya kilimo cha  Mpunga katika kikosi
cha  837 Chita JKT , huku akisema Wizara yake itahakikisha miradi hiyo
inakuwa na tija kwa watanzania kwa kuzalisha mbegu bora.

Akizungumza  kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya umwangiliaji , Waziri Kwandikwa amesema mradi huo
ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na vikosi vya JKT ili kutoa
mchango kwa taifa.

“Tuna mradi wa umwagiliaji, nimefurahi kuona huu mradi ambao tangu
nimepewa jukumu nimekuwa nikiusoma kwenye makaratasi, lakini nilikuwa
na shauku kufika kutokana na mipango ilivyopangwa,nimeridhika na mradi
huu na Wizara itahakikisha inafanya uwezeshaji ili miradi hii isonge
mbele na tukikamilisha mradi huu tutakwenda kulima ekari 12,000 sio
jambo dogo,”amesema.

Amesema watajikita kuzalisha mbegu bora na kuwasaidia wakulima wa
kitanzania kwa kupata mbegu sahihi.

“Wakulima watarajie muda si mrefu sana tutakwenda kuzalisha mbegu za
mpunga, na tutaendelea kufanya utafiti na uzalishaji wa mbegu kwa
ajili ya maeneo mbalimbali, ekari 12,000 sio jambo la mchezo lakini
litapunguza adha kwa wananchi,”amesema.

Akizungumzia mradi wa ufugaji samaki, Waziri Kwandikwa amesema mradi
huo utasaidia vijana wa JKT kupata elimu na kuelimisha jamii kuhusu
mradi huo ambao unatekelezwa kwa gharama za chini.

“Hawa vijana waliopo hapa wanaendelea kupata elimu ya kutosha
kutengeneza miundombinu ya ufugaji wa samaki lakini pia kwenda kueneza
elimu, uzoefu wao natarajia wataenda kutoa elimu yenye tija,
tunatarajia kuzalisha samaki wa kutosha, pia watu tunategemea waje
kujifunza,”amesema.

Ametoa wito kwa watanzania kufanya utalii kwenye eneo hilo kujifunza
kutokana na msukumo uliowekwa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu
Hassan, kwamba watu wajikite kwenye kilimo, uzalishaji.

“Watanzania waone namna tunavyozalisha kwa tija,ukizalisha samaki hapa
una fursa ya kuuza nje ya nchi, na ahadi yangu kama msimamizi wa
Wizara, Wizara itaendelea kuweka nguvu kubwa kuhakikisha miradi hii
inakuwa na tija,”amesema.

Kwa upande wake MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele amesema mradi huo ulianza chini ya mtangulizi wake Meja Jenerali
Charles Mbuge huku akisema  anaendeleza kazi hizo na kwamba lengo ni
kuhakikisha JKT linajitegemea kwa chakula ifikapo mwaka 2024/25.

”Malengo ya JKT ni ifikapo mwaka 2024/25 tujitegemee kwa chakula kwa asilimia 100, ili kuipunguzia serikali gharama za kuwahudumia vijana wa JKT na badala yake fedha hizo zitumike kwenye ujenzi wa miundiombinu ya elimu na afya”amesema

Amesema uzalishaji huo utakapojitosheleza ndani ya jeshi na kuwa na ziada itauzwa kwa wananchi ili jeshi lipate faida zaidi.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Umwangiliaji ,Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena amesema skimu hiyo ni ya aina yake na wamekuwa wakipata ushauri kutoka taasisi mbalimbali za kilimo ikiwamo kituo cha utafiti wa kilimo(TARI).

“Eneo hili ilionekana tusijikite tu na kuzalisha mpunga, bali tufuge na samaki, pia kuna eneo la kujenga kiwanda,ujenzi wa skimu hii ulianza Julai 2020 na ulianza baada ya JKT Makao makuu kuja na wazo la kuongeza uzalishaji ili kulisha vijana wote wanaojiunga na JKT,”amesema.

Amesema ili kuongeza uzalishaji uliandaliwa mpango maalum na kuteua kamati ambayo iliandaa andiko likielezea mpango wa dharura na wa miaka mitano ili kuwa na chakula cha kutosha na kuipunguzia serikali mzigo wa kuhudumia chakula.

Amebainisha kuwa mradi huo unajengwa na wataalamu wa ndani na skimu ya kwanza imejengwa na wazawa ambapo ni wataalamu wa JKT na Tume ya Umwagiliaji na ujenzi wake umefikia asilimia 50.5 na unatarajiwa kugharimu Sh. bilioni 13.1 hadi sasa zimetumika Sh.Bilioni 4.9.

Hata hivyo, amesema kupungua kwa gharama kutokana na kuwepo kwa nguvu kazi JKT ya mitambo na magari yamekuwa yakitumika kwenye ujenzi huo.

Amebainisha kuwa kwa mwaka 2020/21, kikosi hicho kimelima ekari za mpunga 2700 ambapo walipewa malengo ya kulima hekari 1500 na kwasasa wapo kwenye hatua ya uvunaji ambapo tayari ekari zaidi ya 600 zimevunwa na yamepatikana magunia 6713.

“Kilimo cha safari hii kulikuwa na changamoto mvua zilichelewa sana na wakulima wengine jirani wamepata hasara kubwa, na wazo na kutengeneza skimu imesaidia kupata mavuno haya licha ya kuwa bado zoezi la uvunaji linaendelea,”amesema.

Katika ufugaji wa samaki, amesema matarajio ni kuzalisha vifaranga vya samaki 500,000 kwa mwezi na ujenzi umekamilika kwa baadhi ya matenki na mengine ujenzi unaendelea, huku vifaranga 25000 vimeshapangwa kwenye baadhi ya matenki na kwamba kwa ujumla ujenzi umefikia asilimia 30.

Aidha, amesema JKT ina jukumu la malezi kwa vijana, uzalishaji mali pamoja na ulinzi.

“Wapo vijana wa aina mbili wa mujibu wa sheria na wa kujitolea, mafunzo ya kwa mujibu wa sheria yanaendelea katika vikosi mbalimbali na wapo juma la pili sasa, wale vijana wa kujitolea wapo kwenye vikosi mbalimbali ikiwamo hichi, na hivi karibuni kuna kundi lipo hatua za mwisho kwa kupimwa afya na kuhakiki vyeti, baada ya zoezi hilo ile oparesheni ambayo imepatiwa jina la Samia Suluhu, itaanza hivi karibuni,”amesema.