Spika wa Bunge, Job Ndugai akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) na Muongozo wa Kuwajengea Uwezo Wabunge wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu ofisi hiyo ianzishwe nchini. Kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kicheere.
Spika Job Ndugai na CAG Charles Kicheere wakionesha mpango mkakati na muongozo huo.
Watumishi wa NAOT wakifungua champaign
Spika Ndugai, CAG Kicheere na Mhasibu Mkuu wa Hesabu Msaidizi, Aziz Kifile wakinyoosha juu glasi zenye champaign ikiwa ni ishara ya kutakiana heri.
Spika Ndugai (kulia) akisalimiana na aliyekuwa CAG Profesa Mussa Assad wakati wa maadhimisho hayo.
Spika Ndugai akipata maelezo alipokuwa anatembelea mabanda yenye nyaraka mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya watumishi wa ofisi ya NAOT
Baadhi ya wabunge ambao ni wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge wakiwa katika maadhimisho hayo
CAG Kicheere akimkabidhi zawadi Spika Ndugai.
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameitaka Ofisi ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali kujikita katika kuandaa ripoti za ufanisi ili kupata picha juu ya utendaji wa watumishi ndani ya serikali.
Ndugai,aliyasema hayo jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 60, ya ofisi hiyo toka kuanzaishwa kwake.
Amesema kuwa, hivi sasa ipo haja kwa ofisi hiyo kuanza kujikita katika kuanda ripoto za ukagauzi wa ufanisi katika maeneo mbalimbali.
“Ni wakati sasa wakati mnaandaa ripoti hizi za kihasibu lakini pia muanze kuandaa ripoti zinazaohusu ufanisi ili kuondoa malalamiko yanayotoka kwa wananchi”amesema Ndugai
Spika Ndugai amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa pamoja an ofisi hiyo kutoa hati safi lakini bado kuna vitu vinaoneka kuwa haviko sawa.
“Wananchi bado wanalalamika unakuta halmshauri inapewa hati safi lakini wakiangalia hakuna kitu ambacho kipo sawa hivyo ripoti hizi za ufanisi zitasadia kuondoa malalamiko haya kwa kupima utendaji wa watumishi”amesema Ndugai
Pia, amesema Bunge litaendelea kushirikiana na Ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika kujadili ripoti zinazowasirishwa kwa maslahi ya taifa.
Aidha amesema kuwa ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali ni nyenzo muhimu sana kwa Bunge inayolisaidia kuhoji na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Pia tunaomba ofisi yako CAG, kuendelea kutoa elimu kwa waheshimiwa wabunge wetu ili kuwa na mbinu bora za kuhoji mambo mbalimbali katika maneo yao na kuisaidia serikali yetu na Rais wetu”amesema
Pia ameiomba ofisi hiyo kutoa mafunzo kwa wahasibu hasa wa Ofisi ya Rais Tamisemi ambao kwa kaiasi wapo nyuma kutoka na kukosa mafunzo ya mara kwa mara.
“Mnaweza mkawa mnawahuku wahasibu wetu kwa kufanya vibaya katika mahebu lakini ukweli ni kwamba wapo nyuma hasa wale wa Tamisemi hawapati mafunzo ya mara kwa mara”amesema
Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuendelea kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa kuipatia fedha pamoja na rasimali watu.
Hata hivyo Bw.Kichere ameliomba Bunge kubadili muda wa kujadili ripori yake anayoiwasairisha bungeni katika mwaka wa fedha husika tofauti na ilivyo sasa ambapo inajadiriwa mwaka unaofuata.
Aidha amesema kuwa lengo la ofisi hiyo ni kuwa Taasisi ya kisasa kwa kuipindi chake cha uongozi.