Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amefungua Rasmi Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga huku akiweka wazi kuwa Vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga hawana mchakato wala mawazo ya Katiba Mpya zaidi ya kujenga chama na nchi.
Akizungumza leo Ijumaa Julai 2,2021 wakati wa ufunguzi wa shina la wakereketwa na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, Shemahonge amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakina ajenda ya katiba mpya sasa.
“Sisi Chama cha Mapinduzi hatuna ajenda ya Katiba Mpya kwa sasa,huo ndiyo msimamo na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hivi sasa anajenga nchi, anajenga uchumi. Sasa vile vyama ambavyo havina malengo wala ajenda ndiyo vinalazimisha katiba mpya.
“Hivi sasa hatuna mchakato wala mawazo na Katiba Mpya, wazo letu ni kujenga chama na nchi.Sisi vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga tunaungana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwamba mchakato wa Katiba kwa sasa haupo, sasa hivi tunajenga chama, tunajenga nchi iweze kuwa na uchumi tukiangalia uchumi wa nchi yetu umeyumba kutokana na ugonjwa wa Corona ambao umeikumba dunia nzima”,amesema Shemahonge.
Baraka amewataka vijana wa CCM kumuunga mkono Rais Samia Suluhu akisema katika kipindi cha siku 100 amefanya mambo makubwa akionesha kwa vitendo kuwa wanawake wanaweza kuongoza nchi.
“CCM tembeeni kifua mbele kuwa wanawake wanaweza. Rais wetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi. Tuendelee kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu, waaminifu, kumlinda na kulinda amani ya nchi huku tukieleza na kuyasemea mambo mema anayofanya katika kujenga nchi yetu”,amesema Shemahonge.
Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa wa Shinyanga ametumia fursa hiyo kumpongeza kada wa CCM, Edwin Masha Charles kwa kutoa jengo la nyumba yake litumike kama ofisi za Chama Cha Mapinduzi tawi la Negezi kata ya Mwawaza kwa ajili ya shughuli za chama hicho.
“Nimefarijika kuona kijana mwenzetu Edwin Masha Charles kwa kutoa mali yake itumike kwa shughuli za chama. Tunamshukuru kwa kujitolea kukijenga chama. Hii ni kazi ya chama kwani chama kinajengwa na vijana.Najua kuna mambo mengi yataibuka kwamba kwanini amefanya hivi labda anataka uongozi. Nikusihi ndugu ya Edwin usikatishwe tama na maneno ya watu, umefanya kazi ya kizalendo kujenga chama”,amesem Shemahonge.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua mbali na kumpongeza kada wa CCM Edwin Charles kutoa jengo lake litumike kama ofisi ya CCM pia amewaomba vijana kuendelea kujenga chama na kukipambania huku akiwasihi vijana kuendeleza umoja na mshikamano walionao.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu amesema ofisi hiyo ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza itatumiwa na chama na Jumuiya zote za CCM wakati CCM inaendelea na mchakato wa kujenga ofisi zake katika eneo hilo.
Bashemu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa serikali za mitaa pamoja na Madiwani kufanya mikutano ya hadhara na kuwaeleza wananchi kuhusu miradi na kazi wanazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi huku akiwataka vijana kujitokeza kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa shuleni.
Kwa upande wake, Edwin Masha Charles amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kukubali ombi lake la kutoa chumba cha nyumba yake kitumike kama ofisi ya CCM huku akibainisha nia yake ilikuwa ni jengo hilo litumike kwa shughuli za UVCCM kwani tamanio lake ni kuona kila tawi la CCM lina ofisi kwa ajili ya vijana.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifurahia baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akipandisha Bendera ya CCM baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akikata utepe wakati akifungua ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahongenaa viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa nje ya ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye shin la wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
Kada wa CCM Edwin Masha Charles aliyetoa jengo la nyumba yake litumike kama ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Nyandi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza, Suzana Dotto akisoma risala wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (katikati) akiandamana na vijana wa CCM kuelekea kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (katikati) akicheza muziki na vijana wa CCM kuelekea kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog