Afisa Ubora wa Mbolea (TFRA), Bw.Raymond konga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wakiwahudumia wananchi waliofika leo katika banda lao katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************************
Kila Mbolea au kisaidizi cha Mbolea lazima isajiliwe na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kabla haijaanza kutumika nchini kwa mujibu wa kifungu namba 8 cha sheria ya Mbolea.
Ameyasema hayo leo Afisa Ubora wa Mbolea (TFRA), Bw.Raymond konga akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonesho hayo Bw.konga amesema kuwa ili kuweza kujisajili mwombaji anatakiwa kujaza fomu namba moja katika mfumo wa kimtandao wa mbolea unaopatikana kupitia fis.tfra.go.tz. ambapo fomu zitakazojazwa ziambatanishwe maelezo kuhusu matumizi sahihi ya maelezo kuhusu usalama wa mbolea, picha ya kifungashio na sampuli ya mbolea.
Aidha amesema kuwa mwombaji atatakiwa kuambatanisha cheti cha usajili wa jina la kampuni, namba yautambulisho wa mlipa kodi (TIN).
Amesema hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuingiza mbolea nchini isipokuwa awe amepata kibali kutoka katika mamlaka kwa mujibu wa kifungu na.21.
“Uingizaji wa mbolea nchini unafanyika kwa njia mbili ambapo ya kwanza ni kwa kutumia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja.Mfumo huu unasimamiwa na kanuni za ununuzi wa mbolea kwa pamoja, njia ya pili ni uingizaji wa mbolea kwa mfumo huria.Katika mfumo huu kila mtu anaruhusiwa kuingiza mbolea ilimradi amefuata sheria na taratibu za uingizaji wa mbolea”. Amesema Bw.konga.