Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo Joseph Ndalu na kulia ni Afisa Maendeleo ya filamu toka Bodi ya Filamu Bi. Scholastica Mkumbi.
Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali Joseph Ndalu (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu tuzo hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga na kulia ni Afisa Maendeleo ya filamu toka Bodi ya Filamu Bi. Scholastica Mkumbi.
Afisa Maendeleo ya filamu toka Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Scholastica Mkumbi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo hizo Joseph Ndalu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Cosmas Paul maarufu Rapcha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo ) juu ya ushiriki wake siku utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo hizo Joseph Ndalu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali Joseph Ndalu (katikati mbele) juu utoaji wa tuzo hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.
30 Juni 2021
*************************
Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wameahidi kuendelea kuunga mkono kazi mbalimbali za sanaa hapa nchini.
Hayo yamesememwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali.
“Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wenye zamana na Sekta ya Sanaa kupitia BASATA tutaendelea kutoa ushirikiano na wasanii mbalimbali ili kuweza kufanikisha malengo ya kukuza sekta ya sanaa nchini.
Afisa Sanaa Mwandamizi Ndaga ameongeza kuwa kuelekea siku ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali wanataraji kuwa tuzo hizo zitakuwa zitatoa hamasa kwa vijana wengi hapa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali Joseph Ndalu ameahidi kuwa tuzo hizo zitaweka historia kwa kushirikisha wasanii wa tansia mbalimbali.
“Katika tuzo hizi tunatarajia kuwa na wasanii wa tasnia mbalimbali kama wasanii wafilamu, bongo fleva na sanaa mbalimbali hivyo ni imani yangu tuzo hizi zitakuwa za kipekee sana”alisema Bw. Ndalu.
Tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali zitafanyika siku ya jumamosi Juai tatu katika Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.