WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe ,akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Prof.Godius Kahyarara,akizungumza wakati wa Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC) Dkt.Maduhu Kazi,akizungumza wakati wa Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe,(hayupo pichani) wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
Afisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya Stanley Kibakaya,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe (hayupo pichani) mara baada ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) kilichofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa Maafisa biashara nchini kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) kilichofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe,amewataka Maafisa biashara nchini kuacha tabia ya kufunga maduka ya wafanyabiashara wanaodaiawa kwani kufanya hivyo ni kosa sawa na uhujumu uchumi.
Hayo ameyasema leo June 29,2021 jijini Dodoma wakati akifungua semina ya mafunzo kwa Maafisa biashara wa mikoa kilichoandaliwa na kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC).
Waziri Mwambe amesema kuwa kitendo cha Maafisa biashara kufunga maduka ya wafanyabiashara kutokana na kudaiwa mapato au kuisha kwa leseni amesema siyo jambo la busara.
“Unakuta mtu anadaiwa fedha kiasi kidogo tuu labda leseni yake imeisha siku chache zilizopita lakini afisa biashara anafunga duka na kufuri jambo hili ni sawa na ilivyo katika kosa la uhujumu uchumi”amesema Mwambe
Mwambe ametumia semina hiyo kuwaasa Maafisa Biashara hao kutumia taaluma na weledi wao katika kutafuta wawekezaji kwenye Mikoa yao lakini pia kuwa daraja la wawekezaji kuwekeza.
” Nyinyi mna nafasi kubwa ya kuchochea maendeleo kwenye Nchi yetu kama kila mmoja kwa nafasi yake ataamua kwa dhati kutumia weledi na taaluma yake kutafuta wawekezaji.
Nchi yetu ina utajiri sana hakuna sehemu yoyote kwenye Nchi yetu ambayo haina soko la kibiashara, kama siyo Madini basi ni Utalii, Kilimo au hata Viwanda, nyanyueni uwekezaji kwenye Mikoa yenu,” Amesema Waziri Mwambe.
Amesema pia Wizara yake iko katika mpango wa kuwezesha Maafisa Biashara kuwa wasimamizi wa zile asilimia 10 wanazogaiwa makundi maalum ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
” Nafikiri kuna haja ya zile asilimia 10 za makundi maalum ziwe zinasimamiwa na Maafisa Biashara maana haiwezekani Maafisa Maendeleo ya Jamii ndio wasimamie watu biashara wakati siyo taaluma zao,” Amesema Waziri Mwambe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania Dk. Maduhu Kazi, amesema kuwa lengo la semina ya mafunzo hayo ya siku mbili ni kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uwekezaji.
Naye Afisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya Stanley Kibakaya akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Maafisa Biashara wenzake amemuahidi Waziri Mwambe kwamba wataenda kufanya kazi kwa bidii huku wakiwa sehemu ya watekelezaji wa mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo kwa bidii na weledi.
” Tunakushukuru Mhe Waziri kwa nafasi hii uliyotupatia, semina za mafunzo kama hizi zimekua zina manufaa makubwa na tunaomba ziendelee kuwepo mara kwa mara,” Amesema Kibakaya.