Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Lazaro Mwambole akifungua mafunzo kwa wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa mifuko ya Non-Woven na mifuko mingine ya plastiki iliyofanyika leo makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa mifuko ya Non-Woven na mifuko mingine ya plastiki wakifuatilia mafunzo yaliyofanyika makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Lazaro Mwambole akipata picha ya pamoja baada ya kufungua mafunzo kwa wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa mifuko ya Non-Woven na mifuko mingine ya plastiki iliyofanyika makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA EMMANUEL MBATILO
***********************
NA MWANDISHI WETU
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kutilia mkazo kusimamia maswala ya viwango na udhibiti ubora wa bidhaa mbalimbali ikiwemo pamoja na mifuko.
Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Lazaro Mwambole akifungua mafunzo kwa wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa mifuko ya Non-Woven na mifuko mingine ya plastiki iliyofanyika makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa ili kuweza kuzalisha mifuko yenye kukubarika katika masoko lazima izalishwe mifuko yenye ubora inayokidhi matakwa ya viwango husika.
“TBS imekuwa ikihakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo mifuko ya Non-Woven bags, mifuko ya plastiki iliyoruhusiwa zinakidhi matakwa ya viwango kwa mantiki hiyo TBS itaendelea kuhakikisha kwamba biashara zinafanywa katika mifumo inayoeleweka na kukubalika kisheria sambamba na kanuni zinazosimamia mifumo ya viwango na udhibiti ubora”. Amesema Bw.Mwambole.
Aidha Bw.Mwambole amesema ikiwa watumiaji hawawezi kupata bidhaa yenye ubora na inayoendana na mahitaji yake,husababisha kuwepo kwa kwa malalamiko juu ya thamani ya maisha yao na fedha zao.