Na Emmanuel J. Shilatu
Tunaendelea kumulika mambo mengi yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuona namna alivyoupiga mwingi ndani ya siku 100 za utawala wake.
16. Rais Samia ametoa fedha za nyongeza Tsh. Bilioni 322 kujenga barabara za vijijini kupitia TARURA. Sera ya barabara bora kwa kila Kijiji ni turufu ya kihistoria vizazi na vizazi.
17. Rais Samia ameongeza fedha za nyongeza Tsh. Bilioni 125 kukamilisha ujenzi wa maboma ya Madarasa 10,000 kwa shule ya Msingi na sekondari nchi nzima.
18. Rais Samia ametoa fedha za nyongeza Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma ya Zahanati nchi nzima. Hapa Rais Samia amesogeza huduma za afya kwenye kila Kijiji, adui maradhi anakwenda kupigwa vita kivitendo.
19. Rais Samia ametoa fedha za nyongeza Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitenganishani. Kero ya dawa itakwenda kupungua kabisa.
20. Rais Samia amedhamiria kuimarisha maendeleo na kuepusha migogoro kwa Serikali kuu kulipa moja kwa moja posho za mwezi kwa Madiwani katika Halmashauri 168.
21. Katika kuimarisha utendaji kazi, utoaji huduma na kutatua kero za Wananchi, Rais Samia ametoa posho za mafuta ya Tsh. 100,000/= kila mwezi kwa Watendaji kata na Maafisa Tarafa nchi nzima. Hakika Rais Samia ameupiga mwingi sana hapa.
22. Rais Samia ameonyesha nia ya dhati kukuza sekta ya michezo nchini kwa kuimarisha viwanja vya michezo kwa kutoa kodi kwenye nyasi za bandia zinazoingizwa nchini. Hivyo hakuna kodi wala gharama yeyote ile itakayotozwa kwa ingizo la nyasi bandia nchini. Unapozungumzia mafanikio ya michezo ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini.
23. Rais Samia ameimarisha mafunzo stadi kazi kwa Vijana nchi nzima kwa malengo ya kuwaongeza ujuzi wa kiufundi na taaluma. Hii ni njia mojawapo ya utatuzi wa ajira kwa Vijana ambapo sasa watakuwa na uwezo wa kujiajili wenyewe.
24. Rais Samia amedhamiria kumkomboa Msichana kwa kuagiza ujenzi wa shule za Sayansi kwa Wasichana nchi nzima. Lengo ni kuongeza idadi ya Wasichana wataalamu kwenye masomo ya Sayansi nchini.
25. Kama ambavyo Rais Samia anaendelea kuwaamini Vijana kwenye ngazi za mamlaka ndivyo ambavyo anaendelea kuwawezesha Wanawake kwenye madaraka kwa kuwezesha asilimia 50 kwa 50.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
…. Itaendelea …….
*Shilatu, E.J*