Home Michezo DENMARK  YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020,YAICHAPA 4-0 WALES

DENMARK  YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020,YAICHAPA 4-0 WALES

0

DENMARK wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Wales leo Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam nchini Uholanzi.
Mabao ya Denmark yamefungwa na Kasper Dolberg dakika ya 27 na 48, Joakim Mæhle dakika ya 88 na  
Martin Braithwaite dakika ya 90 na ushei na sasa itakutana na mshindi  kati ya Uholanzi na Jamhuri ya Czech.