Home Michezo ITALIA YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020

ITALIA YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020

0

ITALIA imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Austria katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London na sasa watakutana na Ubelgiji au Ureno.
Baada ya dakika 90 ngumu, Federico Chiesa aliifungia bao la kwanza Italia dakika ya 95, kabla ya Matteo Pessina kufunga la pili dakika ya 105 na Sasa Kalajdzic akaifungia la kufutia machozi Austria dakika ya 114.