Wanachama wa Golden Group wakiwapakulia chakula watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali maarufu ‘Golden Group’ kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kimeshiriki chakula cha mchana na watoto wenye mahitaji Maalumu wakiwemo watoto wenye ualbino, wasioona na viziwi cha Buhangija wanaolelewa katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Kikundi hicho cha wanawake wajasiriamali kinachohusika na masuala ya kujikwamua kiuchumi, kusaidiana katika shida na raha pamoja na kusaidia jamii kimeshiriki chakula cha mchana na watoto hao Ijumaa Juni 25,2021.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi, Mwenyekiti wa Kikundi cha Golden Group, Violeth Shirima amesema wameamua kuandaa na kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu ili kuonesha upendo kwa watoto hao.
“Tumefika hapa kwa ajili ya kula ,kunywa na kucheza na watoto wetu ili kuwapa faraja ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi chetu cha Golden Group mwaka 2001. Kikundi hiki kinaundwa na wanachama 16”,amesema Violeth.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Shinyanga, Fransisca Msindu amekipongeza kikundi hicho kwa kuwakumbuka watoto hao akisema wanahitaji faraja.
“Tunashukuru sana kwa ujio wenu, mmewalisha na kuwanywesha vinywaji mbalimbali watoto hawa,namuomba Mwenyezi Mungu awazidishie pale mlipotoa na karibuni sana Buhangija, msichoke kuja”,amesema.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buhangija, Fatuma Jilala mbali na kukishukuru kikundi cha Golden Group kwa kuandaa chakula cha pamoja, amesema shule hiyo ina jumla ya watoto 227 wenye mahitaji maalumu kati yao wavulana ni 115 na wasichana 112.
Wakiwa katika kituo cha Buhangija, wanachama wa Golden Group wamekula chakula na kunywa vinywaji mbalimbali na watoto, kukata keki maalumu pamoja na kuwapatia watoto zawadi kadha wa kadha.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Golden Group, Violeth Shirima akizungumza wakati wa kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group leo Ijumaa Juni 25,2021 ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 ya kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2001. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Shinyanga, Fransisca Msindu akizungumza wakati wa kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group leo Ijumaa Juni 25,2021 ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 ya kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2001
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buhangija, Fatuma Jilala akikishukuru kikundi cha Golden Group kwa kuandaa chakula kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija.
Keki maalumu iliyoandaliwa na Golden Group wakati wa kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga
Mlezi wa kikundi cha Golden Group, Elly Absalom na watoto wakikata keki maalumu wakati wa kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group
Mlezi wa kikundi cha Golden Group, Elly Absalom akimlisha keki mtoto wakati wa kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group
Wanachama wa Golden Group wakiwapakulia chakula watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Wanachama wa Golden Group wakiwapakulia chakula watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Wanachama wa Golden Group wakiwapakulia chakula watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga kilichoandaliwa na Golden Group ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Watoto wakiendelea kupata chakula
Wanachama wa Golden Group wakigawa zawadi ya pipi na chokoleti kwa watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Wanachama wa Golden Group wakigawa zawadi ya juisi kwa watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Wanachama wa Golden Group wakigawa zawadi kwa watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Mwanachama wa Golden Group maarufu Naomi Toto akigonga Cheers na watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Mwanachama wa Golden Group Nsianeli Gelard akigonga Cheers na watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Mwanachama wa Golden Group akigonga Cheers na watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kugonga Cheers na watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Wanachama wa Golden Group wakipiga picha ya kumbukumbu katika kituo cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga
Wanachama wa Golden Group wakipiga picha ya kumbukumbu katika barabara ya Shinyanga – Tinde
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog