****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Rasmi Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFA) kuwakutanisha watani wa jadi Simba Sc na Yanga Mkoani Kigoma mara baada ya leo Simba Sc kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa mkoani Ruvuma na kushuhudia wingi wa mashabiki kuingia kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa aina yake.
Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu tulishuhudia dakika 45 kuisha kwa timu zote kutoka kapa licha ya kosa kosa za hapa na pale kwa timu zote mbili.
Simba Sc ilipachika bao la ushindi katika dakika ya 89 kupitia kwa kiungo wao machachali Luis Miquissone aliyetumia pasi ya Bernard Morrison mara baada ya kucheza mpira wa adhabu karibu na lango la Azama Fc.