Mkuu wa Mkoa mstaafu Injinia Evarist Ndikilo akizungumza na baadhi ya wachezaji pamoja na viongozi mbali mbali wa timu ambazo zilishiriki katika Bonanza hilo ambalo mshindi wa kwanza amejinyakulia zawadi ya mbuzi myama.
*************************
NA VICTOR MASANGU.KIBAHA
Mkuu wa Mkoa mstaafu Injinia Evarist Ndikilo amewataka vijana kuachana na vitendo vya kukaa vijiweni na badala yake wabadilike na kushiriki katika michezo mbali mbali ambayo itaweza kuwapa fursa ya kupata ajira na kujikwamua kiuchumi kupitia michezo.
Ndikiolo ametoa kauli hiyo wakati wa Bonanza maalumu ambalo limeandaliwa na wadau wa kibaha kwa ajili ya kumpongeza kwakazi nzuri ambayo ameifanya wakati wa uongozi wake wa kuwaletea maendeleo wananchi.
Ndikilo katika hotuba yake aliwahimiza wanamicho wote ambao wameshiriki katika Bonanza hilo kuhakikisha kwamba wanaendeleza vipaji walivyonavyo ili kuleta .mabadiliko chanya ya kimaendeleo ikiwa sambamba na kufanyaazoezi kwa ajili ya afya.
Pia Ndikilo aliwapongeza vijana wote wa wilaya ya kibaha ambao wameweza kumualika katika Bonanza hilo ambalo litaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kukuza michezo kuanzia mgazi za Chini Hadi ngazi ya Taifa.
“Kwa kweli leo nimefarika Sana kwa kuweza kupata mwaliko wa Hawa vijana wa Hilo eneo la Garden na wameniomba niwe mwanachama wao na Mimi nimekubali lkn Nia ni kushirikiana na kuleta maendeleo katika mkoa wa pwani.alisema Ndikilo.
Pia aliwahimiza wachezaji hao kuendelea kushikamana kwa pamoja na kuwa na umoja katika suala zima la kuwajibika na kujituma zaidi hususan katika nyanja ya michezo Ili kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia michezo.
Ndikilo ambaye leo alikuwa Mgeni rasmi katika Bonanza hilo aliwahimiza vijana wote.kuhakikisha wanachapa kazi kwa bidii na kuachana na vitendo vya kushinda vijiweni bila ya kufanya kazi.
Naye mratibu wa bonanza Hilo Waziri Manyakala amempongeza Ndikilo kwa kuweza kushirikiana.na vijana pamoja na wananchi katika kuleta chachu ya kimaendeleo.
Pia mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Method Alisema kuwa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ataendelea kushirikiana bega kwa bega katika kukuza sekta ya michezo mbali mbali.
Katika Bonanza hilo ambalo lilijumuisha jumla ya timu nane kutoka wilaya ya kibaha ambapo mshindi wa kwanza kutoka timu ya Halmashauri ya mji Kibaha wakati mshindi wa pili ikienda kwa shirika la ugavi wa umeme Tanesco.