Mkutano wa 14 Baraza la
Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki umefanyika leo tarehe 25 Juni 2021 jijini Arusha huku Mawaziri
wakikubaliana kuendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kilimo ili
kujihakikishia usalama wa chakula kwa wananchi wote Afrika Mashariki.
Mkutano huo ambao ulitanguliwa
na mikutano ya Wataalam na Makatibu Wakuu iliyofanyika jijini hapa kuanzia
tarehe 21 hadi 24 Juni 2021, ulilenga kupitia na kujadili utekelezaji wa
maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya pamoja na kupitia na
kujadili masuala mbalimbali muhimu ya
kisera, kimkakati, miradi na program zinazotekelezwa katika sekta ya kilimo. Aidha, Mawaziri hao wamepokea
na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu kama vile
Taarifa ya Usalama wa Chakula ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu
Mradi wa Afrika wa Kilimo cha Ushindani cha Mpunga kwa Kanda ya Afrika
Mashariki; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Mifugo; Taarifa kuhusu Mradi wa Kuzuia
na Kudhibiti Sumukuvu; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Uvuvi; na Taarifa kuhusu
Uhamasishaji wa Uchangiaji Rasilimali. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano
wa Mawaziri umeongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda na
kuhudhuriwa pia na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa
Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Soud Nahodha Hassan, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Andrew Massawe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid
Tamatama pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Sekta mbalimbali
zinazojishughulisha na masuala ya kilimo na usalama wa chakula hapa nchini.
|
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mhe. Prof. Mkenda akisaini Ripoti ya Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mhe. Prof. Mkenda (kushoto) akiwa na Mawaziri wengine wa Tanzania walioshiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Soud Nahodha Hassan na katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki. |
|
Mwenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa Kenya, Mhe. Lawrence Angolo akizungumza wakati wa Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Kenya katika Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Tanzania, Bw. Patrick Ngwediadi akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamin Mwesiga akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 pamoja na Bibi Jackline Mpuya kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa |
|
Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga (kulia) akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Mkutano ukiendelea |
|
Maafisa Waandamizi wakiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 |
|
Picha ya pamoja |