kushoto ni mkuu wa wilaya mpya wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akikabidhiwa na mkuu wa wilaya aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Richard Kasesela ilani ya CCM ambayo na yeye alikabidhiwa na chama cha mapinduzi alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kutenguliwa uteuzi wake
kushoto ni mkuu wa wilaya mpya wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akikabidhiwa na mkuu wa wilaya aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Richard Kasesela nyaraka za wilaya hiyo ambayo na yeye kwa lengo la kuijua vizuri wilaya hiyo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU mkuu wa wilaya ya Iringa ametakiwa kuhakikisha anatatua changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa gumzo katika wilaya hiyo kutokana na wananchi wa wilaya kuuza ardhi mara mbilimbili na kuvamia baadhi ya ardhi za wawekezaji zenye hati miliki za miaka mingi ya nyuma.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi ya mkuu wa wilaya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa wailaya hiyo imekuwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo mara kadhaa imekuwa ikisababishwa na wananchi wenyewe.
Alimuomba mkuu wa wilaya mpya kuhakikisha kuwa anakuwa makini namna ya kutatua migogoro hiyo kutokana na asili ya wananchi wa wilaya hiyo kwa namna ambavyo wanaishi na kutengeneza migogoro hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi za maendeleo.
Kasesela alisema kuwa licha ya kuwa wilaya hiyo kuna migogoro mingi lakini kuna fursa kubwa kwa wawekezaji kuwekeza kwenye wilaya hiyo ambayo inautajili mkubwa ambao unaweza kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.
Aliongeza kuwa wilaya hiyo ndio kitovu na dira ya mkoa wa Iringa hivyo anapaswa kuwa makini katika namna ambayo anaweza kuongoza kwa kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa wilaya hiyo ambayo kwenye sekta ya michezo hasa mpira wa miguu ambao ndio umekuwa pendwa kwa wananchi wengi wa wilaya hiyo.
Kasesela alisema kuwa wilaya hiyo imekuwa na miradi mingi ya kimaendeleo ambayo inahitaji kusimamiwa kwa umakini ili kufikia lengo la miradi hiyo kuleta maendeleo kwa wananchi na wilaya hiyo.
Alimalizia kwa kumpongeza mkuu huyo wa wilaya kuteuliwa na kumuambia kuwa wananchi wa Iringa wanataka kuheshiwa na kujali muda katika juhudi za kufanya maendeleo,isipokuwa hivyo atapokea majungu mengi ambao yatasababisha migogoro.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa,Mohamed Moyo alisema kuwa ameanza kuitatua baadhi ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa anaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo ili kuhakikisha kuwa anafanikisha kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa kiuchumi na kukuza maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuanzia pale mkuu wa wilaya aliyenguliwa nafasi hiyo.
Moyo alisema kuwa ametokea kwenye chama na yupo tayari kuhakikisha anatekereza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi vilivyo ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Iringa.