…………………………………………………………………….
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Kama kuna timu inayopaswa kutupiwa jicho la pili katika michuano inayoendelea ya UMISSETA basi ni timu ya mpira wa kikapu ya wavulana kutoka visiwani Unguja.
Tayari timu hiyo imekwishatembeza vipigo kwa timu mbili mashuhuri za Tanzania bara ikiwemo Kilimanjaro ambayo leo ilikubali kufungwa vikapu 38-21.
Timu hiyo ya Unguja inayonolewa na Mwalimu Nassoro Salum imekuwa ikitoa burudani safi kwa wakazi wa Mtwara na mikoa ya jirani wanaofurika katika viwanja vya Basketball vya Chuo cha Ualimu Mtwara kushuhudia umahiri wa wachezaji kutoka visiwa vya Unguja.
Katika mechi ya fungua dimba timu hiyo ya Unguja iliifunga Tanga kwa vikapu 48-30.
Mwalimu Salumu anakiri kuwa kinachowasaidia timu yake ni kuwa na wachezaji wazuri wanaopata fursa ya kucheza mara kwa mara katika timu za mitaani huko Zanzibar ukiachilia timu zao za shule.
Matokeo ya michezo mingine ya basketball iliyochezwa leo ni kati ya Geita dhidi ya Kigoma 25-28, Kigoma dhidi ya Dar es salaam 28-101 na Shinyanga dhidi ya Mbeya 60-40.
Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana Songwe walicheza dhidi ya Tabora ambapo Songwe ilifungwa vikapu 15-36, na Ruvuma dhidi ya Iringa, Ruvuma ilishinda kwa vikapu 31-7.
Matokeo ya soka wavulana katika makundi tofauti yanaonyesha Kilimanjaro iliifunga Pwani magoli 2-1, Ruvuma ilikubali kipigo cha magoli 0-3 kutoka kwa Tabora, Mbeya iliifunga Kagera goli 1-0 na Singida ilifungwa goli 1-0 na Arusha.
Mikoa ya Songwe na Shinyanga ilitoka sare ya kufungana goli 1-1, Morogoro iliichapa Simiyu magoli 2-1, Lindi na Dodoma zilitoka sare ya goli 1-1, Katavi ikaifunga Kigoma 1-0, Unguja ikaichapa Rukwa magoli 2-0, huku Mwanza na Njombe zikitoka suluhu, kadhalika kwa mchezo kati ya Tanga na Iringa nazo zilitoka sare ya bila kufungana.
Matokeo mengine ya soka wavulana ni mchezo kati ya Tabora dhidi ya Mtwara ambapo Mtwara ilihinda goli 1-0, Kilimanjaro ilikubali kipigo kutoka kwa timu ya mkoa wa Mwanza baada ya kukubali kichapo cha magoli 0-3, Kagera ikifungwa na Mara kwa magoli 1-2, sawa na mchezo kati ya Songwe dhidi ya Dodoma ambapo Songwe ilifungwa magoli 1-2.
Mchezo kati ya Manyara dhidi ya Iringa ulitoka kwa sare ya goli 1-12, Simiyu dhidi ya Geita 0-0, Katavi dhidi ya Singida 0-3, Rukwa dhidi ya Morogoro walitoka suluhu ya bila kufungana sawa na mchezo kati ya Lindi dhidi Mbeya ambapo walitoka suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo wa Netiboli matokeo Mwanza imeichapa Rukwa magoli 53-7, Geita imeifunga Simiyu magoli 41-19, Mbeya imeifunga Katavi magoli 24-14 na Tanga imeichapa Kigoma magoli 35-20.
Matokeo ya mpira wa mikono wasichana Geita dhidi ya Simiyu 24-17, Shinyanga dhidi ya Morogoro 5-20, Dar es salaam dhidi ya Mbeya 11-15, Unguja dhidi ya Iringa 30-6, Tanga dhidi ya Ruvuma 26-6, na Rukwa dhidi ya Njombe 10-7.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa mikono wavulana Songwe dhidi ya Tanga 10-19, Shinyanga dhidi ya Iringa 16-11, Kagera dhidi ya Rukwa 9-19, Geita dhidi ya Arusha 26-27, Mwanza dhidi ya Ruvuma 29-16, Manyara dhidi ya Pwani 16-24, na Morogoro dhidi ya Tabora 17-20.
Pia Dodoma iliifunga Kigoma 22-20, Mbeya ikaifunga Lindi 32-13, Singida dhidi ya Dar es salaam 16-32, Simiyu dhidi Unguja 12-48 na Kilimanjaro 11-13.