Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki ya CRDB hafla hiyo imefanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akisisitiza jambo kwa washiriki waliohudhuria Uzinduzi wa Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako”iliyozinduliwa na Benki ya CRDB hafla hiyo imefanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akitoa taarifa ya Uzinduzi wa Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako”iliyozinduliwa na benki hiyo iliyofanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodaboda na Bajaji Dodoma Bw.Keneth Chimoti,akitoa neno la shukrani kwa Benki ya CRDB kwa kuzindua Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki hiyo leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakala wa CRDB,Wafanyakazi wa CRDB pamoja na waendesha bodaboda waliohudhuria hafla hiyo wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki ya CRDB hafla hiyo imefanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Nidhamu ya Bodaboda wilaya ya Dodoma Bw.Thobias Humbi,akitoa pongezi kwa Benki ya CRDB kwa kuzindua Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” hafla iliyofanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akiwa ameshika bendera kuashiria uzinduzi wa Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki ya CRDB hafla hiyo imefanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akifurahia na wafanyakazi wa CRDB pamoja na waendesha bodaboda mara baada ya kuzindua Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyofanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa CRDB mara baada ya kuzindua Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki ya CRDB leo June 25,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja na waendesha bodaboda mara baada ya kuzindua Msimu wa pili wa Kampeni yetu ya ”Tupo Mtaani Kwako” iliyozinduliwa na Benki ya CRDB hafla hiyo imefanyika leo June 25,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna,Dodoma
BENKI ya CRDB imezindua msimu wa pili wa kampeni ya ‘Tupo Mtaani kwako’ ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za benki pamoja na kuwaunganisha watanzania walio wengi kutumia huduma za Benki ili kuchochea kasi ya maendeleo.
Akizungumza leo June 25,2021,Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Patrobas Katambi ameitaka Benki hiyo kuishirikisha Wizara ili iweze kutoa maelekezo katika ofisi za Mikoa na Wilaya ili ziwakutanishe na makundi yote ya kina mama,bodaboda,wajasiriamali ili waone jinsi ya kunufaika.
“Katika kipindi cha pili cha awamu hii CRDB tupo mtaani kwako nitaomba sana mtushirkishe pia sisi katika Wizara kwani tutatoa maelekezo katika ofisi za Mikoa na Wilaya ili ziende zikawakutanishe na makundi yote ya kina mama,bodaboda,wajasiriamali na watu wenye mahitaji maalum ili muone jinsi ya kunufaika,”amesema katambi.
Mhe.Katambi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuja na kampeni hiyo kwani anaamini itaweza kutoa ajira kwa vijana wengi nchini kuweza kufika mitaani kuwashawishi watanzania kufungua akaunti.
“CRDB wanatuambia Serikali tunasukuma sera na sheria wajibu tulionao ni kuhakikisha Mabenki yote nchini yanashusha riba katika mikopo na CRDB mmefanya hivyo kuhakikisha kunakuwa na fedha za kuwasaidia wananchi ili kufanya uchumi na kujipatia kipato watoe msaada rafiki.
“Wapo vijana wamefikia katika kada na wameweza kujiajiri wapo watu wazima walikuwa vijana hawa nao wana Programu maalum gharama ni kujaza fomu tu.Wanasema Usione vyaelea ujue vimeundwa,”amesema.
Vilevile,Naibu Waziri amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kutunza fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi katika siku za baadae.
“Athari ya kutokutunza fedha wakati mwingine tuna kasumba ambazo tunazikumbatia wenyewe Mwenyezimungu ametupa fursa nyingi na mabenki mengi lakini sisi hatutaki kuzitumia unapata 100,000 leo kwa dharura unataka kuitumia yote tunza kidogo weka basi hata 50,000 halafu nyingine teketeza hatuna utaratibu wa kutunza fedha,”amesema.
Amesema kazi za Ofisi ya Waziri Mkuu ni kusimamia K tatu ambazo ni kusaidia vijana kufungua mitazamo,na kuhakikisha wanakuwa na ndoto za maisha.
“Tumeenda katika Halmashauri tunatoa fedha kule kama umechukua mkopo nenda CDRD watakusaidia pia wanaweza kukopesha kwa kukuongezea ili ufanye biashara kubwa zaidi pia wamekuwa wakikopesha makundi mbalimbali ya wajasiriamali,”amesema
Kwa upande wake,Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,amesema kampeni ya Tupo Mtaani kwako mwaka jana ilikuwa na mafanikio kwani waliweza kutembelea mikoa 20 na kuwafikia watanzania zaidi ya 100,000.
Amesema mwaka huu wamejipanga kuwafuata wateja pale walipo na kuwapa elimu ya fedha,uhamasishaji wa matumizi ya njia mbadala za utoaji wa huduma na kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba katika malengo.
“Nitoe rai kwa wateja wetu na watanzania kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ya tupo mtaani kwako lengo letu ni kuona tunawafikia watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kunufaika na fursa ambazo zinazotolewa na Benki yao ya CRDB,”amesema.
Pia amesema kuwa kuanzia leo na kuendelea wataendelea kuwepo mtaani kutoa huduma kupitia kampeni yetu ya ‘Tupo Mtaani Kwako.”