Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) akimueleza kuhusu uchunguzi wa kimaabara wa dawa za kulevya unavyofanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa katika Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati Mkuu wa Mkoa akifungua Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma.
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Muhsin Kilonzo (kulia) akimueleza mdau namna uchunguzi wa dawa za kulevya unavyofanyika kupitia maabara baada ya mdau huyo kutembelea banda kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Dawa za kulevya yaliyoanza leo katika Uwanja wa Nyerere Square, Dodoma. Kilele cha maadhmisho ya Siku ya dawa za Kulevya Duniani ni siku ya Jumamosi tarehe 26 Juni, 2021.
Mdau akiwa katika Banda la GCLA Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika jijini Dodoma.