Mchezo mkali na wa kusisimua wa mpira wa kikapu kati ya majirani wawili Songwe dhidi ya Mbeya ambapo Mbeya walishinda vikapu 33-13
Mgeni rasmi katika pambano la mpira wa miguu kati ya timu ya mkoa wa Songwe dhidi ya Pemba ni Mhe Rahma Kassinm Alli ambaye ni Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi akikagua timu hizo kabla ya kuchuana ambapo Pemba ilifungwa goli 1-0.
****************************
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mikoa ya Mwanza na Dodoma imegeuka kuwa tishio kwa wapinzani wao katika mashindano ya UMISSETA inayoendelea katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara.
Michuano hiyo ikiwa katika hatua za makundi, mkoa wa Mwanza ambao ndio bingwa mtetezi wa kombe hilo kwa mchezo wa soka kwa wasichana umekuwa ukitoa vipigo kwa wapinzani wake ambapo katika mchezo uliochezwa leo, timu iyo imeiadhibu timu ya soka wasichana kutoka mkoa wa Kilimanjaro kwa magoli 3-0.
Nayo Singida imeifunga Katavi magoli 3-0 katika mchezo uliochezwa asubuhi katika kundi C, huku Mara ikitoa kipigo kwa Kagera 2-1 na Dodoma ikiifunga songwe kwa magoli 2-1.
Wakati Tabora imeifunga wenyeji Mtwara kwa goli 1-0, timu za Lindi na Mbeya na Rukwa dhidi ya Morogoro zimetoka suluhu. Kadhalika kwa timu za Geita na Simiyu ambazo hadi filimbi ya mwisho ya mchezo timu hizo zilishindwa kufungana, na Manyara na Iringa zilifungana goli 1-1.
Katika mpira wa volleyball wavulana Unguja iliifunga Manyara kwa seti 3-1, Njombe imenyukwa na Singida kwa seti 1-3, huku Songwe ikifungwa na Mtwara seti 0-3 na Katavi dhidi Kagera matokeo ni seti 3-0.
Kwa upande wa mpira wa Volleyball wasichana Arusha ilipata kipigo cha seti 0-3 kutoka kwa Tabora, na Dodoma nayo ilipata kipigo kama hicho kutoka kwa Mbeya.
Matokeo ya mchezo wa mpira wa mikono kwa wavulana Unguja iliinyuka Simiyu magoli 48-12, Songwe ikachapwa na Tanga magoli 10-19, Shinyanga dhidi ya Iringa 16-11, Kagera dhidi Rukwa 9-19 na Kilimanjaro dhidi ya Mtwara 11-13
Mpira wa mikono wasichana Morogoro ikaifunga Shinyanga magoli 20-5, Dodoma na Kilimanjaro zikafungana 12-12, na Tabora dhidi ya Kigoma 12-7
Kwa upande wa mpira wa Netiboli Kilimanjaro imeifunga Kigoma 33-21, Tabora imefungwa na Songwe magoli 26-33, Pwani imeifunga Mtwara magoli 34-15, Singida imefungwa na Shinyanga magoi 27-29, Unguja nayo imefugwa na Ruvuma magoli 21-29 na Dodoma imeilaza Morogoro 26-15