Mkutano ukiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongoza majadilino kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
**********************
Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa (TCM) la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu umefanyika leo tarehe 24 Juni, 2021 jijini Dar es Salaam. Makatibu Wakuu hao wamekutana, sambamba na masuala mengine kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Juni, 2021.
Katika Mkutano huo Mkatibu Wakuu, wamepokea, kupitia na kujadili taarifa ya utekelezaji wa programu, mikakati, miradi, maelekezo na maauzi yaliyotolewa katika Mikutano ya awali ya Sekta hiyo. Vilevile, Makatibu Wakuu hao wamepitia na kujadili agenda zitakazo jadiliwa na Mawaziri katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika hapo kesho. Agenda hizo ni pamo na; kujadili kuhusu mapendekezo ya Taasisi ya Afrika Mashariki juu kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano; kuangalia hatua ya maendeleo iliyofikiwa ya utekelezaji wa miradi na programu katika sekta ndogo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa majini, hali ya hewa na mawasiliano.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya nchini Kenya Bw. Charles Ngunjiri amesema Jumuiya ya Afrika imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa biashara na kurahisha upatikanaji wa huduma mbalimbali katika ya Jumuiya. Aliongeza kutoa rai kwa wajumbe wa mkutano kutumia vyema mkutano huo kutoa michango ya kujenga zaidi itakayo endelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Jumuiya katika sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa.
Katika Mkutano huu wa ngazi ya Makatibu Wakuu, kwa upande wa Tanzania umehudhuriwa na Ndg. Mussa Haji Ali, Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar na Ndg. Amour Hamil Bakari, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar.