Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Pili Hassani akizungumza wakati wa kikao
hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatiwa na
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima
Sehemu ya madiwani wa Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho
Sehemu ya madiwani wa Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amewaambia madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na kupata hati safi kutoka kwa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) isiwafanye kuridhika na kupunguza uangalizi wa fedha za serikali .
DC Hashim aliyasema hayo wakati wa kikao cha Maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokuwa na lengo la kupitia hoja ya mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo alisema fedha hizo zile za Serikali ambazo wanazo ndani.
Kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima
Alisema kwani wanaweza kupata hati safi lakini matumizi yao yakawa hayako sahihi kwa hiyo kuna changamoto zinaweza kujitokeza ambazo hazina athari ukapata hati safi .
“Niwaambie waheshimiwa madiwani pamoja na hati safi tuliopata isiwafanye wakaridhika na kupunguza uangalizi wa fedha za serikali ambazo wanazo ndani niwaombe msimamie na miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mengine itekelezwa kwa kiwango kizuri na watu wakija kupima thamani halisi wakute ipo sawa”Alisema
Aidha kutokana na halmashauri hiyo kupata hati safi kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne aliwapongeza huku akiwataka madiwani hao kuhakikisha wana kuwa mstari wa mbele kufuatilia fedha za serikali ambazo wanazo ndani ili kuhakikisha zinatumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.
“Uzuri DC mlienaye bado ana umri wa kukimbia, kuruka, kucheza naomba tunapokutana huko tukutane kwa ajili ya kazi kwa lengo la kuhakikisha wilaya yetu inaendelea kupata mafanikio makubwa zaidi”Alisema DC huyo.
Awali akizungumza katika kikao hicho cha Baraza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Hassani aliwapongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kutokana na kazi nzuri wanazofanya wamezunguka mkoa mzima lakini Jiji la Tanga wanafanya vziuri na ndio wanaubeba mkoa.
“Katika hili niwapongeza Madiwani kote tulipopita tumebaini kuna changamoto za mapunfufu watendaji kutokutimiza wajibu wetu ipasavyo kukosa umakini kwenye utekeleza wa majukumu yao na hivyo kusababisha hoja nyengine ambazo unapokutana nazo unashangaa…Lakni RC kupitia maelekezo yako unayoyatoa hoja hizo zinaweza kutokuwepo kwenye mabaraza yajayo”Alisema Ras Pili.
Hata hivyo aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanarudisha imani waliopewa na wananchi kwa kuhakikisha wanaisimamia kwa waledi ili iendelea kufanya vizuri.