Mkuu wa wilaya ya Mafia aliyemaliza muda wake ,Shaibu Nnduma akiongea wakati akimkabidhi ofisi Eng. Martin Ntemo.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa wilaya mpya Mafia Eng.Martin Ntemo akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa ofisi wilaya ya Mafia.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa wilaya mpya wa Mafia Eng. Martin Ntemo (kulia) akiwa katika ofisi za CCM wilaya ya Mafia alipokutana na Kamati ya Siasa ya wilayani humo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM (W) Hassan Pango na kushoto ni Katibu wa CCM Kulwa Milonge.(picha na Mwamvua Mwinyi)
***************************
Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
Mkuu wa wilaya ya Mafia ,mkoani Pwani ,Eng.Martin Ntemo amekutana na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilayani humo pamoja na kuzungumza na watumishi na watendaji , kujitambulisha ambapo ametoa vipaombele vyake ili kujiinua kimaendeleo.
Alisema licha ya kupewa maagizo na mkuu wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge kwa wakuu wa wilaya kwenda kusimamia migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi lakini pia atahakikisha anasimamia miongozo ya ilani ya chama cha Mapinduzi na maendeleo ya wilaya kwa kutekeleza miradi kwa maslahi ya jamii.
Atahakikisha wilaya inakusanya mapato kikamilifu ili kuimarisha halmashauri hiyo na kusisitiza kutenga asilimia 10 ya vikundi vya vijana ,wanawake na walemavu.
“Mkabuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato pasipo kujisahau na vyanzo vya kizamani ambavyo vimezoeleka.
Akikabidhiwa ofisi na mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake ,Nnduma ,Eng.Ntemo aliwaeleza anashukuru kuona wilaya imeachwa salama anachoomba ni umoja na ushirikiano ili kuyaendeleza mazuri yaliyoachwa na wengine.
Ameelezwa zipo changamoto mbalimbali ikiwemo za kielimu upungufu wa madawati ,madarasa ,katika afya madawa ,hivyo atasimamia kuhakikisha zinapungua kama si kumalizika kabisa.
Amejipanga kuweka siku maalum ya kusikiliza kero za wananchi kwani itasaidia kuzifikisha katika mamlaka husika na kuzipatia ufumbuzi.
Ntemo aliomba viongozi mbalimbali na watendaji kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano na kumuunga mkono Rais wa sita Samia Suluhu Hassan ili kuifikisha Tanzania mahala pazuri zaidi Kiuchumi .