Kamishana wa elimu,kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Lyabwene Mtahabwa ,akizindua kitabu cha Language Sapportive Pedagogy : Theory,Implementation and Application,hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Kamishana wa Elimu,Kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Lyabwene Mtahabwa akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kitabu cha Language Sapportive Pedagogy : Theory,Implementation and Application,hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WADAU wa elimu nchini wametakiwa kuzitafutia uvumbuzi changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasaidia walimu waweze kufundisha kwa lugha rahisi ambayo itamfanya mwanafunzi aelewe kiurahisi.
Hayo yameelezwa na,Kamishana wa elimu,kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Lyabwene Mtahabwa wakati akizundua kitabu cha Language Sapportive Pedagogy : Theory,Implementation and Application, ambacho kitamsaidia mwalimu kutumia lugha rahisi,inayoeleweka iliyojaa mifano rahisi, picha na vielelezo kuhakikisha mwanafunzi anaelewa dhana.
Amesema kwa ujumla sekta ya elimu inachangamoto nyingi hivyo wadau wa elimu wanatakiwa kuja na suluhisho ni nini kifanyike ili gurudumu la elimu lizidi kusonga mbele.
“Nikishukuru sana Chuo Kikuu cha St John kwa kuona changamoto hii lugha ya kufundishia ni muhimu kwa kitabu hichi naamini watakachokitumia kitawasaidia.Mimi nasema naomba wadau wengine na vyuo viige mfano wa St John vieendelee kutafakari changamoto ambazo zipo na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi,”alisema
Vilevile, amesema harakati zinaendelea katika kuboresha mitaala ya elimu kuhakikisha elimu ya Tanzania inaakisi maisha halisi ya Mtanzania.
“Zipo harakati zinaendelea kuboresha mitaala na pia iweze kuakisi hali halisi mchakato wa wadau umeanza na tutakuwa na kikao lengo kuhakikisha elimu yetu inaakisi maisha halisi ya mtanzania kitaifa na kikanda kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele,”amesema.
Mtahabwa amesema naamini watakaotumia kitabu hicho wataweza kuwa na njia bora ya kuwasilisha darasani.
“Na nimesema unapokuwa na uwezo wa lugha ya kufundishia unakuwa na raha nafsini kwako unakuwa na ujasiri na uwezo wa kuwasilisha kile ambacho umekiandaa kwa watoto kwa ufasaha zaidi lakini kinyume chake kama huna uwezo unakuwa unaogopa utafundishaje na kujibu maswali,”amesema.
Kwa upande wake,Mhadhiri kutoka Chuo cha St John cha Jijini Dodoma,Dkt.Shadidu Ndossa amesema kutokana ufundishaji kuwa ni changamoto walipata mradi wa Language Saporting Teaching and Text Book (LSTT) ambao ulikuwa na lengo la kumsaidia mwalimu kuweza kufundisha kwa lugha ya kueleweka.
Dk.Ndossa ambaye pia ni sehemu ya Wahariri wa kitabu hicho amesema kwa kupitia mradi huo wameweza kutunga vitabu vitatu vya Chemisty,Biology na Hisabati ambavyo vimekuwa msaada kwa wanafunzi na walimu.
Amesema mradi huo kwa sasa unaelekea mwishoni na walimu nane kutoka katika mradi waliweza kuandika kitabu kutokana na kushiriki katika mradi huo
“Ni mradi ambao unahimiza mwalimu kutumia lugha au kuona lugha ni sehemu muhimu kuhakikisha wanafunzi wanaelewa hasa katika masomo ya Sayansi.Kwa mfano mimi katika chapter ambayo nimeiandika kama miongoni mwa waandishi niliandika kuelezea vile vitabu ni namna gani…..
“Vimesaidia kumuunganisha mwalimu,mwanafunzi pamoja na vitabu kwa sababu kumekuwa na changamoto vitabu vinatumia lugha ngumu ikiwa ni pamoja na mifano ambayo haipo katika mazingira ya wanafunzi na tunatumia maneno magumu na sentensi ngumu.
“Kwa hiyo mradi wetu huu pamoja na mambo mengine unahimiza mwalimu kutumia lugha rahisi lugha inayoeleweka lugha iliyojaa mifano rahisi,lugha iliyojaa picha na vielelezo kuhakikisha mwanafunzi anaelewa dhana ambayo inafundishwa,”amesema.
Kwa upande wake,Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St John,Dkt.Zawadi Richard amesema Mradi wa Language Saporting Teaching and Text Book umenisaidia kuweza kuwasaidia walimu waliopo katika shule za Sekondari na hata walimu wenzangu wanaotarajiwa kuwa walimu kujua mbinu za kufundishia.
“Suala la lugha ya kufundishia imekuwa ni tatizo kubwa maana Kiingereza ni lugha yetu ya tatu ama ya pili kwa watanzania lakini jinsi tunavyoendelea kutumia Kiingereza wanafunzi wetu tunaona wanazidi kupata shida.
“Kwa hiyo kupitia Programu hii tumeweza kuwasaidia walimu kwani wameweza kuwafundisha wanafunzi kwa wepesi hii inasaidia wanafunzi kuweza kuimporove kuelewa masomo yao na zaidia walimu waendeleee kujifunza kuwafundisha wanafunzi waelewe,”amesema.
Naye,Mkuu wa Idara ya Somo la Kiingeraza kutoka Shule ya Dodoma Sekondari, Gerald Tibaigana amesema umefika wakati wa kutunga vitabu kwa watu wenye uhitaji maalum ili na wao waweze kupata vitabu vya kujifunzia.
“Na nishauri isiishie katika maeneo ya mijini pia ifike kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum tusiishie kwa wanafunzi ambao wanaweza kuona na kusikia basi tuwafikie hata ambao hawezi kusikia wasioona ili tuweze kufanikisha jambo hili,”amesema
Amesema kupitia vitabu vilivyotungwa ufaulu umeweza kuongezeka kwani awali kulikuwa na changamoto katika ufundishaji kwani wanafunzi wengi walikuwa hawaelewi.
“Nimefarijika sana kuona hili suala ambalo nililitilia mkazo kwakweli kabla ya hapo tulikuwa tunakutana na changamoto kubwa kwa mfano ufundishaji wa somo la Kiingereza ni mgumu sana lakini sasa imetusaidia kuweza kuwasiliana.Tumefanikiwa kwani hata ufaulu umeongezeka na pia hichi kitabu kitaendelea kutusaidia,”amesema Mwalimu huyo.
Kwa upande wake,mwanafunzi wa shule ya Dodoma Sekondari,Vannesa Mwaihojo alikishukuru Chuo cha St John kwa walimu wake kuweza kutunga kitabu hicho ambapo alidai kwa kutumia kitabu hicho kitaenda kuwasaidia kujua lugha inavyoweza kutumika na kutusaidia kuweza kufaulu.