Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani akisalamia jana na viongozi wa Vyama vya Siasa mara baada ya kuwasili Ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani akisaini Kitabu cha wageni jana mara baada ya kuwasili Ofisini kwake.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora(mbele) na viongozi wa Taasisi mbalimbali wakiwa katika Halfa fupi za kuapisha Wakuu wa Wilaya ya Tabora na Kaliua.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani akiwahotubia Wakuu wa Wilaya za Tabora na watumishi wa umma mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya ya Kaliua na Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani(wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja jana na baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya ya Kaliua na Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani (wan ne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya za Tabora na mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya ya Kaliua na Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani (kulia) akimwapisha jana Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Ismail.
Picha na Tiganya Vincent
*****************************
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tabora wameagizwa kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Serikali ili Halmashauri zilizopo katika maeneo ya utawala zifikishe asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Alisema hatua hiyo itafanikiwa ikiwa watazuia mianya ya upoteaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kukusanyia mapato (POS) na kuhakikisha wakusanyaji wa mapato wawe watu wenye maadili na nidhamu
Balozi Dkt. Batilida alisema hayo jana katika hafla fupi ya ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya ya Kaliua na Tabora.
Alisema dhamira ya Serikali ni kuwa Halmashauri zote zinapaswa kujiendesha zenyewe bila ruzuku toka Serikali Kuu kuanzia mwaka 2025 na njia pekee ya kufika huko ni kwa Watendaji wa Halmashauri zote wakabuni vyanzo vipya vya mapato.
Balozi Dkt. Batilida alisema zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri lazima lishirikishe watu wote Watendaji wa Kata, Vijiji, Maafisa Tarafa na Waheshimiwa Madiwani
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kwa mwaka wa fedha 2020/21 Halmashauri za Mkoa wa Tabora zilikadiriwa kukusanya mapato ya ndani kiasi cha Bilioni 25.6 lakini hadi kufikia tarehe 21 Juni, 2021 kiasi cha Bilioni 18.4 sawa na 71.5% zimekusanywa.
Alisema ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri Mkoa wa Tabora sio mzuri kwa kuwa huko wastani wa Kitaifa ambayo ni asilimia 94.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimia Watendaji wa Halmashauri ili waweze kujibu hoja zote walizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG).
Alisema Hamashauri nne Mkoani hapa zimepata hati chafu toka kwa CAG na hivyo ni jukumu lao kuhakikisha makusanyo yote yanapitia mfumo wa Kielekitroniki kwa ajili ya kudhibiti mapato na Matumizi yao.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wakuu hao wa Wilaya wakawahudumie wananchi na kuhakikisha wanatatua kero zote zinazowakabili na kusimamia usalama ili Mkoa uendelee kuwa salama.
Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya zote saba waliahidi kutoa ushirikiano na kumsaidia Mkuu wa Mkoa wa Tabora kutekeleza majukumu yake ya kuuuendeleza Mkoa na kuwaletea maendeleo wananchi ili kudhibitisha imani kubwa aliyopa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika halfa hiyo Dkt. Batilda aliwaapisha Wakuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Yahya Ismail wa Wilaya ya Tabora na Paulo Matiko wa Wilaya ya Kaliua.