……………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge ameingilia kati mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa Mwembengozi kata ya Dutumi pamoja na wizara ya kilimo ,ambapo amehitaji kukaa meza moja na wawakilishi watatu kutoka kwa wananchi na wataalamu wa ardhi, ili kufanya uhakiki na uthibitisho .
Kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi hao ,Kunenge amefika kijijini hapo na kuunda timu itakayokuwa chini ya katibu tawala mkoani hapo.
Alisema ,masuala hayo yanagusa maslahi ya nchi na mtu mmoja mmoja na ustawi wake hivyo yanapaswa kuangaliwa kwa umakini.
“Wananchi hawa nao wana hoja ,hivyo twende kwenye uhakiki na uthibitisho ,naomba mungu anisaidie nitende haki ” alisisitiza Kunenge.
Kunenge alielezea kwamba ,timu hiyo itafanya kazi kwa siku moja ,watahakiki nyaraka ,wataenda kwa hoja kwa kuzingatia sheria ili kupata suluhu na kufanya maamuzi yenye haki ,:”;!Wakati mwingine inahitajika busara na jambo hili litakwisha.
Awali ,mkazi wa Dutumi Fundi Mbegu ,Ramadhani Kondo,Maua Rashid na bibi Zena walisema wapo wenye maeneo hapo tangu mwaka 1968 ,vikiwa ni vijiji vya asili kabla ya ujamaa mwaka 1974.
Walisema ,kijiji hicho cha Mwembengozi kimepimwa ,kipo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ,na katika nyaraka zote hao kilimo hawaonekani katika vijiji vyao sasa wanashangaa wanadai haki ni yao na kutaka kuwapora maeneo yao .
Mbegu alisema ,wakiwa katika eneo hilo ,wizara ilifika kwa wakazi hao kuomba eneo la kupitisha mifugo na sio kujimilikisha.
“Tumelima mikorosho,mihogo ,miembe,mazao mbalimbali ,Sisi hatuondoki haki itendeke ,tumekaa hapa miaka mingi ,na sisi ndio tulikutwa na hao kilimo ikatuomba tuwaonyeshe eneo la kupitisha mifugo ,inakuwaje wanataka tuondoke tena ” walilalamika.
Nae Maua Rashid alibainisha, walifuata ngazi zote kutoa malalamiko yao ambapo mgogoro huo ulimalizwa na mkuu wa wilaya miaka hiyo Halima Kihemba ,na waliishi kwa amani ila amani inataka kuondoshwa baada ya ofisa tarafa kwenda na Kilimo wakidai ni eneo lao na National housing.
Akitoa ufafanuzi ,Kamishna wa ardhi msaidizi mkoani Pwani ,Ruth Kabyemera alieleza,upimaji wa kijiji kitaalamu kijiji kinatangazwa na TAMISEMI .
Ila kisheria wanamtambua aliyekutwa katika ardhi ,kijiji kikimkuta mtu katika eneo hakina haki kwani mwenye haki ni aliyekuwapo toka mwanzo -awali.
Kabyemera alisema ,ufafanuzi huo ni kitaalamu ila hauingiliani na mgogoro uliopo ,hivyo hatua iliyochukuliwa na mkoa itarajiwe kuleta matokeo chanya ili kila mmoja awe na amani .
Migogoro hii ya ardhi ,wakulima na wafugaji huko Kwala ,Dutumi ipo mingi na mkoa kijumla ,kuna kila sababu ya kuishughulikia ili kuipunguza kama si kuisha kabisa .