Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Bw. Abdallah Mwaipaya (kushoto) leo akiwasikiliza Kaimu Meneja wa Utawala wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Asia Shio (wa kwanza kulia) na Bi. Rachel Manyilizu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) alipotembelea banda la kukusanya maoni, ushauri na malalamiko la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), kituo cha JNIA ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) akisalimiana na Maafisa kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo alipotembelea kwenye banda la kukusanya maoni, ushauri na malalamiko ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma lililopo JNIA. Ukusanyaji huo umeanza tarehe 16 Juni, 2021 na itafikia kilele tarehe 23 Juni, 2021.
Meneja Utawala wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Lazaro Matoke akiongea Watumishi wa kiwanja hicho (kulia) waliopo kwenye banda la kupokea maoni, ushauri na malalamiko kutoka kwa watumishi na wadau ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, iliyoanza tarehe 16 Juni na itahitimishwa tarehe 23 Juni, 2021.
Mafundi wa umeme wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kuanzia kulia Bi. Anna Mwenisongole (Fundi Sanifu Mkuu), Bw. Titus Longino na Bi. Jane Tesha wakitengeneza taa za kumwongoza rubani kutua na kuruka vyema kwenye kiwanja hicho
Maafisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda la kukusanya maoni, ushauri na malalamiko la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 16 Juni, 2021 yatafikia tamati tarehe 23 Juni, 2021.