Meneja wa timu ya Bunge SC, Seif Gulamali (kushoto) akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (Taswa SC) nje ya ukumbi wa Bunge mkoani Dodoma.
Meneja wa benki ya Stanbic Tanzania kanda ya Kati Oppi Igolola (kulia) akizungumza na wachezaji wa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo Tanzania (Taswa SC) kabla ya mechi dhidi ya Bunge SC mkoani Dodoma.Taswa SC ilishinda mabao 5-1.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya waandishi wa habari za michezo (Taswa SC) Majuto Omary (Kulia) akijaribu kumtoka mshambuliaji wa timu ya Bunge SC, Festo Sanga. Taswa SC ilishinda mabao 5-1.
Wachezaji na timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wadhamini wao, Benki ya Stanbic kabla ya mechi maalum ya kirafiki dhidi ya Bunge SC. Taswa SC ilishinda mabao 5-1.
………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam.
Timu za mpira wa miguu na netiboli za Bunge la Tanzania (Bunge SC) na ile ya waandishi wa habari za michezo (Taswa SC) sasa zitakuwa zinacheza mechi ya kirafiki kila mwaka.
Taswa SC ilifanya ziara ya siku tatu mkoani Dodoma baada ya kufuatia mualiko wa Bunge SC na kucheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa Jamhuri.
Katika mechi hizo, Taswa FC ilishinda mabao 5-1 dhidi ya Bunge FC upande wa soka kwa upande wa netiboli, Bunge Queens iliofunga Taswa Queens 32-12.
Katibu wa Bunge SC, Waziri Kizingiti alisema kuwa wamevutiwa na uamuzi waandishi wa habari kujishughulisha na michezo kwa vitendo na kuwataka mabali ya soka, pia wawe na timu ya riadha, kuvuta kamba na michezo mingine.
Kizingiti alisema kuwa hatua hiyo itawafanya waandishi na wabunge kushiriki katika michezo hiyo mbali ya mpira wa miguu na netiboli.
“Hali hii itachochea maendeleo ya michezo nchini na hasa ukizingatia kuwa Bunge SC inapokea maombi mengi ya michezo ya kirafiki na kuelemewa na ratiba.
Safari hii tulikuwa na maombi mengi, tukatoa nafasi kwa timu chache na nyingine zitakuja kikao kijao cha mwezi Novemba. Taswa SC tumewapa heshima na tumefarijika kukutanao nao mbali ya matokeo,” alisema Kizingiti.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza timu hiyo ya Bunge kwa kufanikisha na wadhamini wao, benki ya Stanbic kwa kufanikisha ziara hiyo ambayo imewawezesha waandishi kujifunzu masuala mbalimbali ya shughuli za Bunge.
“Tumefarijika kukutana na Wabunge wetu na vile vile kubadilishana mawazo, Taswa SC itatumia ushirikiano huu kuhamasisha maendeleo ya michezo Tanzania. Naamini tutafikia malengo yetu chanya. Naipongeza pia benki ya Stanbic kwa kutuwezesha na kukutana na Wabunge,” alisema Majuto.