NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
WAAJIRI kutoka sekta ya Umma na Binafsi mkoani Morogoro wameelezwa kuwa moja ya majukumu yao ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo vitokanavyo na kazi kwa kuzingatia sheria ya usalama na afya mahala pa kazi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi (WCF) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani humo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini kutoka WCF Dkt. Abdulsalaam Omar alisema wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waajiri mkoani Morogoro kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Juni 22,
2021.
“Mfuko
huu umeundwa kwa dhumuni la kukidhi matwakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu
fidia kwa wafanyakazi na kukuza mbinu kuzuia ajali, magonjwa ama vifo ni moja
ya matwakwa hayo.” Alifafanua Dkt. Omar
Aliwaambia
washiriki kuwa Mfuko umekuwa na faida kubwa kwa wafanyakazi, waajiri na taifa
kwa ujumla ambapo kwa sasa wafanyakazi wana uhakika wa kinga ya kipato kutokana
na majanga yasababishwayo na ajali, magonjwa au vifo vitokanavyo na kazi.
“Hali
kadhalika waajiri nao wanapata muda zaidi wa kushughulikia masuala ya
uzalishaji na uendelevu wa biashara zao kwani mfuko ndio unaobeba jukumu la
kugharamia pindi mfanyakazi anapoumia, kuugua aama kufariki kutokana na kazi”
Alifafanua na kuongeza…..Wafanyakazi nao wanapata utulivu kazini kutokana na
kupungua kwa migogoro hasa pale ajali zinapotokea sehemu za kazi nah ii inasaidia
sana kuongeza tija na uzalishaji nah ii inachangia kuongeza pato la taifa.
Akiwasilisha
mada kuhusu Usalama na Afya Mahala pa Kazi, Meneja Tathmini za Vihatarishi
Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi alisema ili kuzingatia sheria ya usalama na
afya mahala pa kazi waajiri hawana budi kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi
kwa kuwapatia wafanyakazi vifaa vya kujikinga (Protective gears) na wahakikishe
wanavitumia ipasavyo.
Ili
kuonyesha madhara ya kufanya kazi bila ya kuvaa vifaa vya kujilinda, Bi. Naanje
aliongoza washiriki kufanya onyesho la athari za ulemavu uliotokanao na kazi ambapo
washiriki watatu walivaa uhusika wa ulemavu wa kukatika vidole vya mikono na
hivyo wakawa na wakati mgumu wa kutumia mikono hiyo kula chakula.
Wakizunguzma kwa nyakazi tofauti baada ya kupata mafunzo hayo, washiriki walisema yamekuwa ni yenye manufaa makubwa kwao na bila shaka watatumia elimu waliyoipata ili kuhakikisha wanatekeleza vema jukumu la kuweka mazingira salama kwa wafanyakazi mahala pa kazi.
“Tusiridhike na tusibweteke na Mfuko kwa kusema midhali WCF ipo basi masuala ya usalama na afya mahala pa kazi iwe sio kipaumbele chetu la, tusifanye hivyo, Fidia iwe ni kitu cha mwisho ije pale tu inapohitajika hakuna namna mtu ameumia au amepata ugonjwa basi aweze kupata fidia.” Alisema Iddi Fuko, Meneja na Usalama Mahala pa Kazi, Unitrans Tanzania Limited, Morogoro.
Alisema mafunzo hayo yasibaki kwa washiriki tu bali yaende hadi kwa maofisa na wafanyakazi wa ngazi za chini ili elimu hiyo iweze kuwasaidia wengi.
“Mafunzo haya yamenipa motisha kubwa kwa kutambua masuala ya usalama mahala pa kazi, lakini pia tumefundishwa umuhimu wa kulinda viungo vyetu na hivyo yatupasa kuweka mazingira mazuri mahala pa kazi ili kupunguza ajali na magonjwa kazini.” Alisema Dotto Ramadhani, kutoka Haki Hoteli Morogoro.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini kutoka WCF Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati) akiwa na Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Madai Mwandamizi, Bw. Silvanus Kuloshe, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani Morogoro kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi na shughuli za Mfuko Juni 22, 2021.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi 9WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, akifungua mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo waajiri mkoani Morogoro umuhimu wa kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ili kupunguza vihatarishi sehemu za kazi. Mafunzo hayo yamefanyika Juni 22, 2021 mkoani Morogoro
Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Mfawidhi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani Morogoro Bw. Kasian Baraka tayari kuanza mafunzo hayo.
Bi. Naanjela Msangi
Bi. Naanjela Msangi