Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakikata
nyasi kwa ajili ya kwenda kutengenezea vikapu. (Picha na John Dande).
Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakiandaa nyasi kwa ajili ya kushonea vikapu.
Mkazi wa Kijiji cha Ikando Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Maria
Muhema, akishona moja ya kikapu kwa ajili ya kuweza kuviuza.
halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe, Furaha Kilasi, akishona moja ya kikapu kwa ajili ya kuweza kuviuza
kujipatia riziki.
Picha ya
pamoja baada ya kumaliza kushona vikapu hivyo.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Washonaji wa
vikapu Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe wameiomba serikali
kuwatafutia soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao za vikapu ili kuweza kuleta
tija.
Wakizungumza
na waandishi wa habari washonaji hao wamesema wanakabiliwa na changamoto ya
kukosa soko la uhakika na hivyo kulazimika kuuza bila ya faida.
Mmoja wa
washonaji hao akiwemo Maria Muhema (61) mama wa watoto watano mkazi wa kijiji cha
Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe,amesema ameanza kazi ya ushonaji vikapu
tangu akiwa msichana ili kujipatia kipato lakini soko hilo limekua likizunguuka
maeneo yao tu hivyo kushindwa kunufaika kwa sababu ya kuuza kwa mazoea.
“Elimu ya
ushonaji vikapu tulifundishwa na mzungu alitokea Njombe mjini na nilianza tangu nikiwa msichana kipato chake bado ni
kidogo,lakini ninavyofikiri tukipata mateja nje ya mkoa wetu tutanyanyuka
kiuchumi”amesema Maria.
Alisema kuwa
wateja wapo lakini bado malighafi za kutengenezea bidhaa hizo kama nyasi zimekua changamoto kupatikana.
“Kutengeneza
hivi vikapu tunatumia nyasi ambazo zinaota kando ya mto lakini wakati mwengine
zinakua mbali hivyo tunalazimika kununua kwa vijana ambao wanatuuzia shilingi
10,000 ambapo ukilinganisha na uuzwaji wake wa kusuasua tunapata
hasara”amesema.
Naye Furaha
Kilasi (39) mkazi wa kijiji cha Ibumila hlamshauri ya wilaya ya Njombe ni mama
watoto watatu amesema suluhisho la bidhaa hiyo kuwa na thamani ni kutafuta soko
la nje kwa sababu la ndani halijabadilisha maisha yao.
“Nina watoto
ninasomesha kupitia kazi hii lakini tunapata kidogo sana,tunaamini tukipata
soko la nje bei ya kikapu itaongezeka….ugumu wa maisha ndio ulionifanya nishone
vikapu lakini sasa bei haiendani na uandaaji wake ambapo kikapu kinaanzia
shilingi 4000 hii sio nzuri kwetu”amesema Kilasi.
Kwa upande
wa Sayuni Kaduma (26) mkazi wa kijiji cha Ikando halmashauri ya wilaya ya
Njombe,mama wa mtoto mmoja alianza kushona vikapu tangu akiwa mtoto amesema
soko la vikapu sio rafiki kwa sababu bei zake ziko tofauti.
“kwa siku
tunashona vikapu kimoja au viwili,bei ziko tofauti soko sio zuri unakuta mteja
anakuagiza bidhaa ukimpelekea anaanza kujishushia bei au anakwambia havina
ubora wakati huo sapo ulishamtumia pamoja na bei zake”amesema Sayuni.
Pia Sayuni
ameiomba serikali kuwaunga mkono kwa kuitambua bidhaa hiyo kwa kuwatafutia soko
la nje pamoja na kuwatambua katika mikopo ya halmashauri ya asilimia tano za
wanawake.