Afisa Rasilimali
Watu wa Kiwanda cha Tanga Pharmaceutical and Plastic Limited (TPPL) Jenipher Mburuja kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Pongwe Dkt Ummykulthum Kipanga kwa ajili
ya kusaidia kambi ya upasuaji wa pua, masikio na koo katika halfa iliyofanyika kwenye kituo hicho kushoto anayeshuhudia ni Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya Pongwe Bahati Shiminogeni
Afisa Rasilimali
Watu wa Kiwanda cha Tanga Pharmaceutical and Plastic Limited (TPPL) Jenipher Mburuja kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Pongwe Dkt Ummykulthum Kipanga kwa ajili
ya kusaidia kambi ya upasuaji wa pua, masikio na koo katika halfa iliyofanyika kwenye kituo hicho kushoto anayeshuhudia ni Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya Pongwe Bahati
Shiminogeni

Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
KIWANDA cha Tanga Pharmaceutical and Plastic Limited (TPPL) leo
wametoa msaada wa vifaa tiba katika
kituo cha Afya Pongwe Jijini Tanga vyenye thamani ya Sh Milioni 2.4 kwa ajili
ya kusaidia kambi ya upasuaji wa pua, masikio na koo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni Endotracheal Tubes 100, Syringe
10 CC 1000,Syringe 5CC 1000,Syringe 2 CC 1000 na JIK Tablets 5000 ambavyo
vitasaidia katika utoaji wa huduma kwenye kituo hicho.
Akizungumza wakati akikabidhi Msaada huo,Afisa Rasilimali
Watu wa Kiwanda hicho,Jenipher Mburuja alisema kiwanda hicho kimetoa msaada huo
ikiwa ni katika kurudisha kwa jamii inayowazunguka ambapo wamekuwa wakifanya hivyo
kwenye kusaidia masuala mbalimbali.
Alisema
baada ya kupokea maombi ya ufadhili kwa ajili ya kambi ya upasuaji wa
Pua,Masikio na Koo waliona ni muhimu kuwasaidia msaada huo
wa vifaa ili kuweza kufanikisha kambi hiyo ikiwa ni
kuondosha changamoto ambazo zinaweza kujitokeza wakati wakiendelea na
zoezi
hilo.
“Tulipopokea maombi ya ufadhili wa Kambi hiyo kwa ajili ya
vifaa tiba vya upasuaji wa pua,masikio na koo na tukiwa kama wadau wa afya
tukaona tununue vifaa hivi vyenye thamani ya milioni 2.4 kwa ajili ya kuwasaidia
uponyaji wa magonjwa hayo “Alisema Mburuja ambaye ni Afisa Rasilimali Watu wa
Kiwanda cha (TPPL)
Aidha alisema pia katika
kurudisha kwa jamii inayowazunguka kiwanda hicho ambacho ni wadau wakubwa wa
Elimu,Usalama na Afya,wametoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo kujenga
banda la watoto la kliniki kituo cha Afya Makorora,Benchi la kukalia wagonjwa
kituo cha Afya Duga,wamewakatia Bima ya Afya ya NHIF wanafunzi walemavu 83
Pongwe.
Afisa Rasilimali huyo alisema pia walikwisha kununua viti vya
kusubiria wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwemo
kutoa vitanda 20,magodoro 20 na shuka 20 katika kituo cha Afya Duga ikiwemo
friji la kuhifadhia damu kwenye kituo cha Afya Pongwe.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo ,Mganga Mfawidhi wa
Kituo cha Afya Pongwe Dkt .Ummykulthum Kipanga alishukuru kwa msaada huo ambao wamepatiwa
na kiwanda hicho huku akieleza umefika wakati muafaka kwani na Tanga kuna tatizo
la Koo na Pua ambalo linapelekea watu kwenda Dar kwa ajili ya kufuata matibabu .
Alisema baada ya kuliona hilo waliwaomba madaktari bingwa
wafike kwa ajili ya kufanya upasuaji kwenye kituo hicho na kiwanda hicho hakikuweza
kuwaacha nyuma waliwashika mkono kufanikisha jambo hilo.
Naye kwa upande wake Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya Pongwe Bahati
Shiminogeni alisema wamefurahi sana wao kama watumishi kwa vifaa hivyo hasa Jik
ambayo ni gharama kubwa ukiangalia kopo moja bei yake ni elfu 65000.
Bahati alisema msaada huo ni mkubwa ambao wamewapatia kwa
ajili ya vifaa vitakavyotumika kufanya upasuaji wa koo,pua na masikio kwa wananchi watakaofika kupata huduma ya matibabu hayo