Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel, akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka (hayupo pichani) wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya za mkoa huo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo June 22,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,akisaini kiapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi,akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka (hayupo pichani) wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya za mkoa huo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo June 22,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi,akisaini kiapo.
Wakuu wa wilaya wakila kiapo cha utii na utumishi na kuilinda nchi mbele ya Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati Bi.Jasmin Bakari.
MKuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,akizungumza mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi,,akizungumza mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya ,akizungumza kwa mara ya kwanza tangu ahamishiwe Chamwino kutoka wilaya ya Uyui Mkoani Tabora hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
MKuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi,hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
MKuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma leo June 22,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma huku akiwataka kusimamia elimu, viwanda na kilimo ambavyo ni vipaumbele vya mkoa huo.
Wakuu wapya wa Wilaya walioapishwa leo June 22,2021 jijini Dodoma ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa,Remidius Emmanuel na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Khamis Mkanachi ambao waliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wiki iliyopita.
“Ninyi ni wawakilishi wa Rais Samia ambaye amewaamini na kuwapa nafasi miongoni mwa wengi ambao wanahitaji nafasi hizo, sasa msilewe madaraka na kusahau majukumu yenu,” amesema
Ameeleza kuwa Dodoma vipaumbele vyetu ni vitatu lakini kikubwa katika elimu tunataka tukafanye mapinduzi na ninyi ndio wawakilishi wa Rais hakikisheni katika wilaya zenu mnasimamia kikamilifu.
Mtaka amesema Mkoa wa Dodoma bado uko chini katika sekta ya elimu ambapo katika matokeo ya kitaifa hakuna shule za Dodoma katika shule bora 100.
Mtaka amewataka wateule hao kujikita kusikiliza kero za wananchi na kujenga mahusiano baina ya ofisi ya mkuu wa wilaya na viongozi wa makundi mengine wakiwemo viongozi wa dini na Chama.
Aidha RC Mtaka amewataka Wakuu hao wa Wilaya kutokuwa na balehe ya madaraka kwani ni mbaya na itawafanya wasifanikiwe katika mipango yao.
“Nawashauri msiwe na barehe ya madaraka, kuona ninyi mmeshakuwa matawi ya juu hamtaki kushirikiana na watu wengine, katika ulimwengu huu kila mtu ana umuhimu wake hakuna aliye juu zaidi ya mingine,” ameeleza
Mtaka amewataka kuwa makini na aina ya marafiki ambao watawapata kwani wengi ni feki na wanawafuata sababu ya vyeo vyao.
“Moja ya faida mtakayoipata nyinyi ambaye ni wateuliwa ni kupata watu feki unafanya ujinga anasema jembe letu hakuna kama wewe na uzuri wa madaraka unapata marafiki feki.Jitahidi umeintaini uhalisia mimi namba yangu ya simu ndio nilitumia tangu naanza kumiliki simu.Kwahiyo nimementaini simu yangu moja kwa sababu nimeona viongozi wengi akiombwa simu anasema anaomba inayopatikana.
“Sisi marafiki wa majina tunakwambia ukweli ila marafiki wa vyeo vyetu hawezi kutuambia ukweli.Nimentaini marafiki zangu wale wa cheo nimeaacha Simiyu na wale wa jina bado nipo nao mpaka leo message yangu hapa ni kwamba acheni epukeni balehe ya madaraka .
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel, amemshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kumuamini kutekeleza kwa nguvu yale yote ambayo atatakiwa kutekeleza.
“Namshukuru Rais Samia kuniamini mimi kijana miongoni mwa vijana wengi kwa kunipa nafasi, nitailinda imani yake kwangu kwa kusimamia na kutekeleza yale yote ambayo yananipasa nitekeleze bila kuvunja sheria,”amesema
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Khamis Mkanachi,, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwa atashirikiana katika kuhakikisha anatekeleza adhima yake ya kuibadilisha Dodoma na kuifanya kuwa ya viwanda.
“Dodoma ni makao makuu ya nchi, lazima tuhakikishe tunashirikiana na mkuu wa mkoa kuhakikisha tunaboresha huduma zote za kijamii zikiwemo elimu, maji na kujenga viwanda kila wilaya ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana wetu,”amesema