Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokutana leo Juni 22,2021 katika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 22,2021, alipokua akielekea Nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya SADC unaotarajiwa kuanza kesho.