Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro akila kiapo mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Adam Malima mapema leo jijini Tanga.
Picha na Ahmed Mahmoud Tanga
***************************
Mkuu wa mkoa wa Tanga amewaapisha wakuu wa Wilaya wapya wapatao wanne
kati ya nane waliochaguliwa na mh rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan
Wakuu hao walioamishishwa vituo vya kazi na kwenda katika Wilaya za
Tanga ni pamoja na Hashim Mgandilwa mkuu wa Wilaya Tanga ,Ghaibu
Bullet lingo, mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mh Abel Yeji Busalama, Mkuu
wa Wilaya kilindi Mh Siriel Shaidi Nchembe, Mkuu wa Wilaya Handeni .
Wapya ni Basila kalubha Mwanukuzi Mkuu wa Wilaya korogwe, kalisti
Lazaro Bukhay Mkuu wa Wilaya Lushoto, na Halima Abdallah Bulembo kuwa
mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga .
Akizungumza mara baada yakuwaapisha wakuu hao wa wilaya Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Adam kighoma Ali Malima amewasisitiza wakuu wa Wilaya wote
kufanya kazi kwa kufuata maadili na kujiepusha rushwa na kuvaa mavazi
ya heshima kujiepusha na unywaji wapombe kupitiliza,
Aidha kwa mujibu wa Malima aliwataka kutokutembea na watoto wa shule
na wenye umri mdogo pia kujifanya miungu watu na kuchukua Mali za
wananchi kwa kutumia nguvu kinyume na maadili ya uongozi.
Amesisitiza pia wakuu wa Wilaya kujikita katika kutatua migogoro ya
wananchi kuafuata katika makazi yao na sio kusubiri viongozi wa juu
kufika katika Wilaya zao pia kusimamia kilimo kwani mkoa wa Tanga
unategemea kilimo kwa kiasi kikubwa.
Aliwataka Kuakikisha halmashauri zote zinakusanya mapato ya kutosha na
kusaidia jamii ikiwemo vijana na kina mama kupata asilimia kumi
zilizowekwa kisheria na kusaidia katika kujikimu na maisha na mikopo
ya riba nafuu.
Kwa upande wao wakuu wa Wilaya walioapishwa na kula kiapo wamesema
kwamba wapo tayari kuwatumikia wananchi na kufuata maadili ya utumishi
wa umma na sio vinginevyo na kamwe hawatamuangusha Mh.Rais.
Akiongea Mara baada ya Kuapishwa mapema Asubuhi Kalisti Lazaro Mkuu
wa Wilaya ya Lushoto amesema Wilaya yake itahakikisha inakuwa kwa kasi
hususani katika sekta ya elimu afya na miundo mbinu ya barabara pamoja
na Wilaya kuwa na maendeleo ya haraka kwa kutumia ilani ya chama cha
mapinduzi ambayo walielezea kwa wananchi kutatua matatizo yote
yanaowakabili