Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akizungumza wakati akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akizungumza wakati akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akizungumza wakati akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude (kushoto) Kahama Festo Kiswaga (katikati) na Shinyanga Jasinta Mboneko wakiwa ukumbini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Phileomon Sengati akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi (kushoto) na wadau mbalimbali wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuteua viongozi wachapakazi katika mkoa wa Shinyanga akisema matarajio ya Wana Shinyanga ni maendeleo tu.
Salum Mbuzi ameyasema hayo wakati akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa wilaya za Kishapu (Joseph Modest Mkude), Shinyanga (Jasinta Mboneko) na Kahama (Festo Kiswaga) iliyofanyika leo Jumatatu Juni 21,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
“Sisi tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia kutuletea timu nzuri ya kimkakati wa maendeleo ndani ya mkoa wetu wa Shinyanga. Mhe. Mkuu wa Mkoa Dkt. Philemon Sengati, hapa nilikuwa nikitafakari nikiangalia sura zenu, halafu nilikuwa namtafakari Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alivyopanga timu hii, kwa kweli Wana Shinyanga tuna bahati sana”,amesema Salum Mbuzi.
“Mimi mkuu wa mkoa tuliyenaye ni ndugu yangu, namfahamu vizuri sana, ni mchapakazi kweli kweli lakini mheshimiwa Mkuu wa mkoa tumepata bahati kubwa haya majembe (Jasinta Mboneko, Festo Kiswaga na Joseph Mkude), ni wachapakazi wazuri”,ameeleza Salum.
Amemuomba Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na wakuu wa wilaya na viongozi wote kubuni mbinu mbalimbali za kuleta maendeleo akisema Shinyanga haina majungu na Wana Shinyanga wanachokitaka ni maendeleo tu.
“Kwa hiyo sisi tunawakaribisheni Shinyanga lakini tunawaombeni sana jambo tunalolihitaji kutoka kwenu, kutoka serikali yetu, Shinyanga isibakie nyuma , tunataka Shinyanga iendelee”.
“Mhe. Rais Samia amewateua na kuwaleta hapa, sisi tutawapa ushirikiano wa hali ya juu lakini sisi Wana Shinyanga tunahitaji maendeleo. Na sisi pamoja na kwamba serikali ina mikakati lakini sisi pia tuwaambieni tu kuwa pia tunayo mikakati, Shinyanga tutaiendeleza sisi wenyewe tuliomo humu ndani pamoja na nyinyi viongozi”,amesema.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, Shinyanga haina Uwanja wa ndege, tunahitaji uwanja wa ndege, Shinyanga sisi wafanyabiashara tunakwamishwa na uwanja wa ndege ‘Airport’, kwanza ni ushamba kuwa na mkoa ambao hauna Airport (Uwanja wa ndege), hata ule wa uwanja wa Kahama nao ni wa Kishamba shamba tu, lakini tutajenga uwanja mpya hapa Shinyanga”,amesema Salum.
Hata hivyo amewaomba viongozi wa mkoa wa Shinyanga na wananchi kwa ujumla kuwa wazalendo kwa kutumia bidhaa za Jambo katika shughuli mbalimbali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mbeneko amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kumwamini kutumikia nafasi hiyo katika wilaya ya Shinyanga huku akieleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati amewakaribisha Wakuu wa wilaya walioteuliwa na Mhe. Rais Samia mkoani humo huku akiwataka kwenda kutatua changamoto za wananchi bila kuchoka waendeleze mazuri ya mkoa wa Shinyanga.
“Matarajio yetu ni makubwa sana kwenu , naamini mtasimamia biashara na uwekezaji ikiwemo kulinda wawekezaji wadogo. Tunataka kuona wilaya zetu zinapaa kiuchumi.Mkasimamie halmashauri katika kusimamia mipango mbalimbali ya maendeleo”,amesema Dkt. Sengati.