Home Mchanganyiko RAIS SAMIA ATEUA WAJUMBE 6 WA BARAZA LA USHINDANI

RAIS SAMIA ATEUA WAJUMBE 6 WA BARAZA LA USHINDANI

0

………………………………………………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua  wajumbe sita (6) wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal- FCT) kwa  mujibu wa kifungu cha 83(2) (b) cha Sheria ya Ushindani (The Fair Competitionn  Act). Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo: 

  1. Dkt. Onesmo Michael Kyauke kutoka Locus Attoneys;
  2. Prof. Honest Prosper Ngowi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe; 3. Dkt. Hanifa Twaha Masawe kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe;
  3. Mhandisi Bonifasi Gissima Nyamo-Hanga kutoka Wakala wa Majengo Tanzania; 5. Dkt. Godwill George Wanga kutoka Baraza la Taifa la Biashara; na 6. Dkt. Neema Bhoke Mwita kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania

Uteuzi wa Wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe  16, Juni, 2021.