Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Kardinali Polycarp Pengo mara baada ya kuwasili katika maadhimisho ya ibada ya misa takatifu ya jubilei ya miaka 50 ya upadre wa Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo,iliofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa fatima – msimbazi centre Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akishiriki ibada ya misa takatifu ya jubilee ya miaka 50 ya upadre ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo,iliofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa fatima – msimbazi centre Dar es salaam, kushoto kwa makamu wa rais ni mkewe mama Mbonimpaye Mpango na kulia ni Mwanasheria mkuu wa serikali Prof. Adelardus Kilangi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Akimkabidhi Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo zawadi ya cheti cha shukran kilichotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya kumpongeza kwa utumishi uliotukuka.
Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo akiwasha mshumaa kuashiria mwanga uliomuongoza katika miaka yote ya utume wake katika kanisa ikiwa ni jubilei ya miaka 50 ya upadre wake iliofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa fatima – msimbazi centre Dar es salaam.
Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo akiongoza ibada ya misa takatifu ya jubilei ya miaka 50 ya upadre wake. Maadhimisho hayo yamehudhiriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakimkabidhi Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo zawadi ya Monstrance ambayo hutumiaka katika ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu na Baraka kuu ikiwa ni siku aliotimiza miaka 50 ya Upadre.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, Maaskofu kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na viongozi wa serikali mara baada ya kukamilika kwa ibada ya misa takatifu ya jubilei ya miaka 50 ya upadre ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na waumini waliojitokeza katika Jubilei ya miaka 50 ya Upadre ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo iliofanyikia katika Parokia ya Bikira Maria wa fatima – Msimbazi Centre Dar es salaam
PICHA: OFISI YA MAKAMU WA RAIS.