Home Biashara WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI RASIMU YA SERA...

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI RASIMU YA SERA YA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGO NA BIASHARA NDOGO

0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo leo jijini Dar es Salaam.

Dk. Consolatha Ishebabi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Wizara ya Viwanda na Biashara akiwasilisha rasimu kwa wadau wa sekta binafsi kabla ya kuanza kwa majadiliano kwa washiriki.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Alfred Mapunda akizungumza jambo katika warsha hiyo.

Irene Mlola Mkurugenzi Mtendaji FSDT akitoa mchango wake katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Wadau mbalimbali wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara wakjadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam.

WADAU wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara leo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo huku ikiwa ni mchakato wa maboresho wa sera hiyo muhimu nchini.
Akizungumza na wadau hao wakati akizindua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashil Abadallah amewataka washiriki hao kupitia kwa makini rasimu hiyo na kutoa mapendekezo yatakayoiboresha zaidi ili kupata sera inayokidhi mahitaji na hasa katika dunia ya leo.
Dk. Abdallah amewataka wajumbe waliopata fursa hiyo kuhakikisha wanatoa maoni bila kujipendelea wao pekee, bali kwa kuzingatia maslahi ya wajasiliamali wote.
Aliwataka kutambua kuwa Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo’ nchini inayoandaliwa ibabeba wajasiriamali zaidi ya milioni 4.5 hivyo inaitaji umakini katika maandalizi yake ili kuja na suluhisho ya changamoto nyingi kwa wajasiliamali.
“Kwa bahati nzuri zaidi, sekta hii ndio inayobeba takribani asilimia 98 ya viwanda vyote nchini. Hii ni faraja kwa kuwa malighafi za nchi yetu hasa za wakulima zinapata masoko katika viwanda hivyo hasa ikizingatiwa viwanda vya sekta hii vimesambaa nchini kote na vingi vikijihusisha katika uongezaji thamani hasa wa mazao ya kilimo,” alisema.
Aidha Naibu Katibu Mkuu alibainisha kuwa Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa sekta binafsi nchini hususan thamani ya uendelezaji wajasiriamali katika kuendeleza shughuli za uchumi wa nchi.
Alisema sera za nchi zimeweka bayana nafasi na jukumu la sekta binafsi katika shughuli za moja kwa moja za uzalishaji na kufanya biashara.
“Dira ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya 2020 -2025 na Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano wa Maendeleo, pamoja na mambo mengine zinatilia mkazo kuishirikisha ipasavyo sekta binafsi katika kuendeleza au kukuza jasiriamali katika kukuza biashara zinazochochea mauzo ya nje ili kuleta uwiano wa maendeleo,” alisema.