Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako akifuatilia mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akifuatilia mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Bw.Suleiman Ame amemuakilisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles E. Msonde akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako amewataka wadau wa Elimu nchini kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa mitaala ya Elimu ngazi ya Awali,Msingi na Sekondari yatakayosaidia kuboresha Elimu nchini.
Hayo ameyasema leo tarehe 18/06/2021 katika Mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya uboreshwaji wa mitaala nchini.
Amesema kufuatia uwepo wa malalamiko mengi kuhusu mitaala ya Elimu nchini ipo haja ya kuhusisha wadau kutoa maoni ya maboresho.
“Nawaomba muwe huru katika kutoa maoni kwa sababu itasaidia katika kufanya Elimu nchini kuwa bora” amesema.
Waziri Ndalichako amesema kuwa mpaka sasa nchi imeshafanya mabadiliko ya mitaala kwa mara tano,na kama hatafanyika mwaka huu yatakuwa ni mara ya sita hivyo amesema wadau waeleze watakachoona kinafaa katika kuboresha mitaala.
Aidha amesisitiza kuwa mabadiliko ya Mitaala ya sasa yanapaswa kuendana na Serikali iliyopo madarakani ambayo imejikita katika ukuaji uchumi kupitia viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amesema kuwa matarajio ya mkutano huu, ni kupatikana kwa uelewa wa pamoja wa Mitaala iliyopo sasa na kupokea maoni ya Elimu na Mitaala itakayorekebishwa.
“Na imani kuwa tutapata maoni mengi yatakayoboresha Elimu yetu nchini,hivyo tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha tunafanikisha ubora wa Elimu” amesema Dkt.Aneth.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian, amesema taasisi hiyo umejipanga kuhakikisha inaboresha mitaala kuendana na mahitaji ya sasa.
Jumla ya wadau 700 wa Elimu Tanzania wamejumuika pamoja katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa maoni ya uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya ngazi ya Awali,Msingi na Sekondari