Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Bw. Kajubi Mukajanga kwenye kikao chao na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,(hayupo pichani) wakati akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,amewataka watanzania na vyama visivyo vya kiserikali kulinda haki za binadamu na kufuata sheria za uhuru wa kujieleza kwani ni jukumu lao kikatiba.
Pia amesema kuwa jukumu la serikali ni kuhakikisha inasimamia na kuzilinda sheria hizo kupitia taasisi ya tume ya haki za binadamu na utawala bora.
Prof.Kabudi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI).
Amesema katika kuhakikisha kila Mwananchi anakuwa na uhuru wa kupata habara serikali imeridhia mikataba wa Afrika 1981 ambapo ibara ya 9 inaeleza kwamba kila mtu anahaki ya kupata taarifa na kila mtu ana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake.
“Tanzania iliridhia mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966 na juni 1976 ambapo ibara ya 19(1) inaeleza kuwa kila mtu anahaki kuwa na maoni yake bila kuingiliwa, kila mtu ana haki ya kujieleza ikijumuisha na kuomba na kupata habari.
Prof.Kabudi amezikakikishia asasi zisizo za kiraia na mashirika yanayosimamia Uhuru wa kujieleza na haki ya kupata taarifa kama utekelezaji wa ibara ya 18 ya katiba.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Bw. Kajubi Mukajanga amesema kuwa sheria ya ATI ilipitishwa na kutiwa saini na Hayati Rais John Magufuli Septemba 23, 2016.
Amesema Malengo ya sheria hii ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa kuainisha wigo wa taarifa ambazo umma una haki ya kuzipata kukuza uwazi na uwajibikaji wa wenye taarifa; na kuainisha mambo mengine yahusianayo na hayo.
“Sheria hii inatoa uhai kwa haki ya kikatiba ya kupata taarifa, na inaeleza taratibu za kutumiwa na wananchi kupata taarifa, huku ikiweka shuruti kwa maafisa wa serikali na taasisi zinazotumia rasilimali-fedha ya umma kutoa taarifa muhimu kwa wananchi bila kusubiri kuombwa,
“Lakini pamoja na nia hii njema, uhalisia ni kwamba utekelezaji wa sheria umekuwa ukisuasua na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi haujaimarishwa kama inavyokusudiwa na sheria,”amesema
Mukajanga amesema tafiti zilizofanywa na taasisi za Twaweza (2017) MCT (2019) pamoja na MISA-Tan (2020) zilibainisha kwamba raia wengi hawana ufahamu wa sheria hii, japo wanakubali kwamba taarifa zinazoshikiliwa na serikali ni rasilimali ya umma