>
Kulia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi
Kaali Akimkabidhi Mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu katika Skimu ya
Kilimo cha Umwagiliaji Madibila Bw. David Noble Mkurugenzi wa Kampuni ya
Ukandarasi ya White City International.
Bw. Shabani Sawasawa (mkulima) akizungumzia manufaa ya Mradi wa Regrow katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji ya Madibila, iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali. |
· ·
MKANDARASI AKABIDHIWA KAZI
· >
LENGO NI KUKUZA UTALII NA UCHUMI KWA
KANDA YA KUSINI
Na: MwandishiWetu – Madibila
Ujenzi
na ukarabati wa miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji katika skimu ya
Madibila iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali Mkoani Mbeya, umeanza
rasmi kwa mkandarasi kukabidhiwa eneo la ujenzi wa mradi na mkataba kwa
utekelezaji wa mradi huo, ambao unalengo la kusimamia ustahimilivu wa
maliasili kwa ajili ya ukuaji wa utalii na shughuli mbadala za kiuchumi
kusini mwa Tanzania.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daudi Kaale,
amesema Tume hiyo inajukumu kubwa la kusimamia kilimo cha umwagiliaji
nchini na kuhakikisha kwamba Skimu ya kilimo kama ya Madibila inafikia
malengo yaliyokusudiwa.
“Uzoefu unaonesha kuwa serikali imejenga
skimu nyingi kwa gharama kubwa lakini baada ya muda hazitekelezi kazi
zake au majukumu kama ilivyokusudiwa, tija na uzalishaji kupungua na
hata mundombinu kuharibika.” Alisema Kaale.
Alisisitiza kuwa
kuanzia sasa ni hazma ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa
miundombinu yote inarejea katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi
katika malengo yaliyokusudiwa, ili kuongeza pato la Taifa, kuondoa
umaskini na kuhakikisha ongezeko la ajira kwa wananchi.
Akiongea
katika makabidhiano hayo msimamizi wa Mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji Mhandisi Mkuu Ebenezer Kombe amesema,yeye kama Msimamizi
Mkuu,anajukumu la kusimamia ubora, gharama halisi za ujenzi na muda wa
miezi 18 ambao umepangwa kwa kazi kukamilika.
Kwa upande wake
Muwakilishiwa Mkandarasi kampuni ya wazawa White City Internatinal,
Bwana. David Noble amesema, wakulima watapata nafasi ya kuendelea na
shughuli zao za kilimo wakati ujenzi ukiendelea, na watajitahidi kufanya
kazi kwa kiwango na wakati.
Bw.Shabani Juma Sawasawa ni mkulima
katika eneo hilo,amesema kuwa, ujio wamradi utakuwa na manufaa ya
kuokoa upotevu wa maji baada ya ujenzi wa mfereji wenye urefu wa
kilometa tatu kukamilika “Wakulima tutanufaika na kutunza maji pamoja na
kuyaruhusu yaende katika mto Ruaha Mkuu kwa matumizi ya viumbe hai
wengine, Maliasili na Mazingira.”Alisisitiza
Mradi huo wa REGROW
ni Mradi wa usimamizi stahimilivu wa maliasili kwa ajili ya ukuaji wa
utalii na shughuli mbadala za kiuchumi kusini mwa Tanzania, Mradi ambao
unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania.