Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia) akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba wakiwasili katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo akizungumza katika hafla hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Nae Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba (kulia) wakisimama kwaajili ya wimbo wa Taifa katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba wakitia saini katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba (Kushoto) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba wakibadilishana mikataba katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba (kushoto) pamoja na Nae Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba wakionesha mikataba katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo amesema Serikali haina mpango wa kuhamisha jukumu la uandishi wa vitabu na uandaaji wa mitaala kutoka kwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Kwa sababu hiyo amewataka waandishi binafsi wa vitabu vya Kiada na Ziada kwa shule za Msingi na Sekondari kushirikiana na TET katika kufanya uandishi bora kwa maslahi ya taifa hili.
Dk. Akwilapo amesema hayo leo Juni 17. 2021 wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya uratibu na uandishi wa vitabu 32 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari kati ya TET na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi za TET jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba, Mkuu wa DIT, Profesa Praksedis Ndomba, wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wa taasisi hizo na watumishi wa taasisi hizo.
“Jukumu la kuandaa mitaala na kuandika vitabu lipo chini ya TET hili lilikuwa chachu ya uanzishwaji wa taasisi hii lakini likaondolewa mwaka 1992 na hapo sasa waandishi mmoja mmoja wakawa wanaandaa vitabu kwa ajili ya watwoto wetu.
Amesema ni jambo la kawaida kwa serikali kutumia rasilimali ilizo nazo mahali ambapo rasilimali hizo zipo.
“Kwa mantiki hii, TET watatumia rasilimawatu kutoka DIT kufanikisha malengo yake. DIT nao kupitia ushiriki huu kwenye kazi ya Uandishi wa Vitabu vya Kiada vya Masomo ya Ufundi watakuwa wametekeleza lengo lake la kusaidia jamii,” amesisitiza Dk. Akwilapo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba amesema kuwa taasisi imeshakamilisha kazi ya kuandika na kusambaza vitabu vya kiada vyote kwa ngazi ya elimu ya awali na msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba kwa shule zinazotumia kiingereza na kiswahili kama lugha za kufundishia.
Hata hivyo amesema kuwa TET imezingatia upatikanaji wa vitabu vya kiada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu yaani wasioona na wenye uoni hafifu.
“Kwa kundi hili TET imeshasambaza vitabu vya kiada hadi darasa la tano na kwasasa inakamilisha kazi ya kuchapa vitabu vya Breli na vyenye maandishi yaliyokuzwa ambavyo ni mahsusi kwa wanafunzi wenye uoni hafifu kwa darasa la sita na la saba”. Amesema Dkt.Aneth.
Sambamba na hayo amesema kuwa kwa upande wa Sekondari, Taasisi imekamilisha uandishi wa vitabu vya kiada 45.Kati ya hivi vitabu 16 ambavyo ni Geographia kidato cha kwanza na pili, Kiingereza kidato cha kwanza na cha pili, Historia kidato cha kwanza na cha pili, Fizikia kidato cha tano na sita, Chemia kidato cha tano na sita, Biolojia kidato cha tano na sita, Basi Applied Mathematics kidato cha tano na sita, Kiswahili kidato cha tano na sita na tayari vipo shuleni.
Pamoja na hayo amesema kuwa wataendelea kuandika vitabu vya masomo ya ufundi kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT). Vitabu hivyo vitaandikwa kwa kutumia mihtasari iliyoboreshwa ya mwaka 2019.
“Vitabu hivyo ni vya masomo yote nane ya shule za ufundi ambayo ni Engineering Science, Civil Engineering, Surveying, Architectural Draughting, Building Construction,Woodwork and Painting, Mechanical Engineering na Electronics and Communication Engineering kidato cha I-IV”. Amesema Dkt.Aneth
Nae Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba amesema kazi ya kuandika vitabu 32 kwa masomo 8 ya elimu ya ufundi kwa shule za sekondari imekuja kwa wakati muafaka na kwamba itasaidia katika kuoanisha elimu wanayoipata kutoka ngazi ya sekondari hadi kuingia katika vyuo na Taasisi za ufundi hapa nchini.
“Na hapa nisisitize kuwa kazi hii tutaifanya kwa weledi na umakini mkubwa kwani tunao wataalamu waliobobea katika elimu ya ufundi,” anasema Profesa Ndomba.