Mwakilishi wa Wordvision Tanzania ,Agatha Matumaini akizungumza wakati wa Kongamano hilo |
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ajari Mwarimwengu akizungumza wakati wa kongamano hilo |
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga akizungumza wakati wa Kongamano hilo |
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Mkinga Sosten Mtena akizungumza wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa 2021 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo. |
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo
SEHEMU ya wanafunzi wakiandamana wakati kongamano hilo
MIMBA
za Utotoni, Ubakaji, Ulawiti na ukosefu wa elimu ya jinsi ya afya na
uzazi ni miongoni mwa vikwazo vinavyowakabili watoto wa kike wilayani
Mkinga mkoani Tanga.
Hayo yalisemwa na Afisa Ustawi wa
Jamii wilayani Mkinga Sosten Mtena wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto
wa Africa 2021 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani
humo.
Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la World Vision
Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Mkinga
lililowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za
msingi, walimu na wazazi.
Alisema kwamba vikwazo vingine ni
usafirishaji haramu wa watoto kwenda nchi jirani ya Kenya kutoka Bukoba
ikiwemo kuchomwa kwa watoto vitendo ambavyo vinapelekea kukosa haki zao
za msingi.
“Kwa mfano Mimba za Utotoni (katika mwezi Machi 2020
hadi may 2021) Jumla ya kesi 37 za Mimba ziliripotiwa jambo ambalo
linakwamisha watoto kushindwa kutimiza ndoto zao hivyo niiombe jamii
ibadilike”Alisema
Afisa Ustawi huyo alisema ili kuweza kumaliza
vitendo vya namna hiyo lazima jamii ibadilike na kuachana tabia hiyo
ikiwemo kuvikemea visiweze kujitokea wakati mwengine.
Hata hivyo
alieleza watoto waliopo katika mazingira hatarishi kwa kunyimwa haki
zao ni wanaoishi na wazee sana,wanaishi na walezi,wazazi ambao
hawajiwezi,walio kwenye mapigano au vita,ambao ni wakuu wa kaya,watoto
wa kike,wamitaani ,yatima na wale ambao wanafanya kazi viwandani au
migodini.
“Lakini zipo athari zinazowakabili watoto ikiwemo
unyanyasaji na uzalilishaji, watoto kutumikishwa kingono, kutekelezwa,
kunyimwa kwenda shule au kupekekwa shule na mila na desturi potofu zenye
madhara kwa watoto”Alisema
Awali akizungumza wakati wa
kongamano hilo,Mwakilishi wa Wordvision Tanzania ,Agatha Matumaini
aliwaomba viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja
kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto na inapotokea mtoto anafanyiwa
vitendo vya ukatili watoe taarifa bila kujali lolote.
“Kwani
inakuwa ni vibaya na inauma watoto anafanyiwa ukatili na mzazi
anashirikiana na mhalifu kuweza kumaliza hilo suala jambo kimya kimya
huo ni ukatili kama ilivyo mwengine”Alisema
Alisema Shirika hilo
kwa kushirikiana na wadau ikiwemo serikali na halmashauri kwenye kamati
za ulinzi wa mtoto wameweza kusaidia kwenye mambo ya afya na lishe.
Hata
hivyo alisema watoto 75 walikutwa wana shida lakini kwa ushirikiano wa
afya na shirika hilo watoto waliweza kuwekewa mfumo maalumu wa kulishwa
na baadae kurudi kwenye hali zao za kawaida na wanaendelea vizuri.
Naye
kwa upande wake Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mkinga Erick Farahani aliwataka
wazazi na walezi kuungana kwa pamoja kukataa na kumekea vikali vitendo
vya ukatili kwa watoto ambavyo vinawakwamisha kufikia ndoto zake
“Pamoja
na kukemea kwa muda mrefu vitendo vya kikatili ,viovu kwa watoto lakini
bado vinaendelea hivyo wataendelea kuvikemea na kuvikataa kwa nguvu
zote kwa lengo la kuhakikisha vinatoweka kwenye jamii “Alisema
Hata
hivyo alisema pia wanapigana na vitendo vya watoto wadogo kuuza bidhaa
ndogo ndogo ikiwemo maandazi,ndizi na katika muda ambao walitakiwa kuwa
shulenijambo ambalo linawanyima haki yao ya msingi kupata elimu bora.
“Lakini
suala la Ubakaji,Mimba za utotoni bado tunavikataa na katika hili
nawaomba wazazi na walezi tuungane kwa pamoja kukataa na kumeea maana kumeibuka tabia kunapotokea mtoto amepewa mimba
wanamalizina kifamilia badala ya kuacha sheria ichukue mkondo wake hivyo
lazima tulikatae na kulipinga”Alisema