Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021 kijiji cha Chihanga. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na kushoto kwake ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. Wa tatu kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo na wa pili-kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Mhandisi Styden Rwebangira.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji na Kata ya Chihanga, nje kidogo ya jiji la Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji na Kata ya Chihanga, nje kidogo ya jiji la Dodoma (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kijiji na Kata ya Chihanga, nje kidogo ya jiji la Dodoma (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021. Kulia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangira (kushoto) na Meneja wa TANESCO Kanda ya Kati, Mhandisi Frank Chambua (kulia) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, uliofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga (kulia) na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde (kushoto) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, uliofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Ceylex Engineering (PVT) LTD, wakitambulishwa mbele ya wananchi na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, uliofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021. Kampuni hiyo ndiyo itakayotekeleza Mradi husika.
Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, uliofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, iliyofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akijadiliana jambo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde muda mfupi kabla ya Waziri kuzindua rasmi Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa pili-kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kushoto kwa Waziri), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (katikati) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Mhandisi Styden Rwebangira (kushoto kwa Mwenyekiti) wakifurahi pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi, baada ya Waziri kuzindua rasmi Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, katika hafla iliyofanyika kijiji cha Chihanga, Juni 16, 2021.
………………………………………………………………………………………………….
Na Veronica Simba – REA
Serikali inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi za Kitanzania takribani bilioni 17.3 kuwafikishia umeme wateja wa awali 4,609 kupitia Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alibainisha hayo jana, Juni 16, 2021 alipokuwa akizindua rasmi mradi huo katika hafla iliyofanyika katika kijiji na kata ya Chihanga, nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Alisema kuwa Mradi huo utatekelezwa katika kata 16 za Mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miezi 12 ambapo fedha za utekelezaji wake zimetolewa na Serikali kwa asilimia 100.
“Tunawaomba wananchi watumie nishati ya umeme katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za afya, elimu, maji, mawasiliano na kuboresha thamani za bidhaa za kilimo cha viwanda,” alitoa hamasa Waziri.
Aidha, Waziri Kalemani alibainisha kuwa Mradi huo hauna fidia hivyo akawataka wananchi ambao wako katika maeneo inakopita miundombinu husika, kutoa maeneo yao pasipo kudai fidia kama mchango wao katika miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine, Waziri alisisitiza kuwa bei ya kuunganisha umeme wa njia moja kwa wateja wote nchi nzima iwe kijijini au mjini ni shilingi 27,000 tu kutoka shilingi 177,000 ya awali na kwamba kwa wenye kuhitaji kuunganishiwa umeme wa njia tatu, gharama yake ni shilingi 139,000 kutoka shilingi 912,000 iliyokuwa ikitozwa awali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka aliwataka wananchi kutumia umeme huku wakiuunganisha na maendeleo pamoja na elimu.
“Nyumba tunazoweka umeme tufanye maendeleo. Tuone saluni pamoja na kufunga taa ili kuwawezesha watoto kujisomea na kukuza ufaulu mashuleni,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, alimhakikishia Waziri kuwa wananchi wa Chihanga wako tayari kulipia shilingi 27,000 ili waunganishiwe huduma hiyo kwa ajili ya kuutumia katika kukuza kipato na kujiletea maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo alibainisha kuwa, Mradi huo uliozinduliwa na Waziri Kalemani ni sehemu tu ya mpango mkakati wa Wakala ambao umelenga kusambaza umeme katika maeneo yaliyo pembezoni mwa miji na majiji.
Wakili Kalolo aliongeza kuwa Mradi huo utatekelezwa katika mikoa mitatu ambayo ni Arusha, Mwanza na Dodoma ambapo utaongeza uwekezaji katika nyanja mbalimbali za maeneo yaliyo pembezoni mwa miji ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda na biashara mbalimbali.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga alieleza kuwa gharama za kutekeleza Mradi huo katika mikoa yote mitatu ya Arusha, Mwanza na Dodoma ni takribani shilingi bilioni 31.2 ambapo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 12.