Home Mchanganyiko RC MAKALLA KUUNDA MKAKATI WA KUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA...

RC MAKALLA KUUNDA MKAKATI WA KUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

0

****************************

NA EMMANUEL MBATILO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla amesema hivi karibuni ataunda mpango kazi wa kuhakikisha Mkoa huo kuwa safi na kuwatengenezea mazingira mazuri wamachinga.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ziara yake kwenye Wilaya ya Temeke na kukutana na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe.Makalla amesema ameandaa mpango umeoanisha changamoto ambazo zinakwamisha usafi katika Jiji la Dar es Salaam.

“Tunapokea wageni kutoka nchi mbalimbali lakini Dar es Salaam haipo vizuri kwasasa, kuanzia Airport mpaka Mnazi Mmoja kuna vibanda, takataka, watu wanapika na wanatupa uchafu hovyo hii ni aibu”. Amesema Mhe.Makalla.

Aidha Mhe.Makalla amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia zoezi la usafi katika maeneo yao ili kuweza kuondokana na uchafuzi wa mazingira katika mkoa huo.

Amesema katika mpango huo kuna changamoto ya ufanyaji wa biashara kihorera katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

“Kuna changamoto ya elimu, watu hawajahamasishwa kuhusu suala pa usafi kwamaana hawajaelimishwa namna ya kutunza mazingira na kuondokana na uchafuzi wa mazingira kuanzia nyumbani anapoishi”. Amesema Mhe.Makalla.

Sambamba na hayo Mhe.Makalla ameshangazwa kuona gereji nyingi barabarani katika maeneo ya Tandale ambazo zinaashiria uchafuzi wa mazingira.

Hata hivyo amewataka TARURA kushirikiana na madiwani katika miradi ya maendeleo kwenye eneo husika.