**************
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka Miss East Africa 2021, yanatarajia kufanyika Novemba, mwaka huu, jijini Dar es Salaam na kushirikisha nchi 15.
Makamu wa Rais wa mashindano hayo Jolly Mutesi alisema ni fursa nzuri kwa Tanzania ina kujitangaza kupitia utalii na uwekezaji na kwamba yameandaliwa Rena Events Limited ya mkoaniDar es Salaam.
Mutesi ambaye yupo nchini kwa ziara wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya awali alisema, mashindano hayo ni makubwa ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakitarajiwa kuangaliwa na watu wengi duniani.
Alisema mashindano hayo yayarishwa mibashara kupitia televisheni, akitoa wito kwa makampuni mbalimbali yanayohitaji kutangaza biashara zao ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kupitia mashindano hayo.
Mutesi alizitaja nchi washiriki kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Djibouti na Tanzania.
Nyingine ni Somalia, Madagascar, Malawi, Ushelisheli, Sudan Kusini, Comoro na Mauritius.
Mashindano hayo yalibuniwa na kuanzishwa na Rena Callist yalianza mwaka 1996 na kuwahi kufanyika Burundi kwa udhamini wa Hayati Rais Piere Nkurunzinza.
“Kuanzia sasa mashindano ya Miss East Africa yatakuwa yakifanyika kila mwaka, yatasaidia katika kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, kukuza utalii, kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji,” alisema Mutesi.
“Mashindano pia yatatoa elimu na kusaidia katika changamoto mbalimbali hasa zinazowakabili wanawake na watoto wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki