**********************
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mashindano ya UMITASHUMTA yanayoendelea katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara yameingia katika hatua ya robo fainali ambapo miamba ya michezo mbalimbali itaanza kuonyeshana kazi hapo kesho.
Mratibu wa Mashindano hayo Leonard Thadeo amesema maandalizi yote yamekamilika ambapo washindi wa michezo mbalimbali wamekwishajulikana.
Timu zilizoingia hatua ya robo fainali kwa upande wa soka wavulana ni Geita, Shinyanga, Dar es salaam, Tanga, Mara, Rukwa, Tabora, Tabora na Mtwara.
Kwa mujibu wa Thadeo, timu ya mkoa wa Geita itapambana na Shinyanga, Dar es salaam itavaana na Tanga, Mara watapambana na Rukwa na Tabora itachuana na Mtwara.
Kwa upande wa soka maalum wavulana Kilimanjaro watachuana na Kigoma, Dar es salaam watapambana na Tabora, Mtwara itachuana na Njombe na Singida itachuana na Shinyanga.
Katika soka wasichana Tabora itachuana na Lindi, Dar es salaam dhidi ya Singida, Geita dhidi ya Mara na Mwanza dhidi ya Kagera.
Timu zitakazokutana hatua ya robo fainali katika mpira wa wavu ni Mbeya dhidi ya Mwanza, Dar es salaam itacheza na Katavi, Mtwara dhidi ya Mara na Pwani dhidi ya Dodoma.
Kwa mpira wa mikono timu zilioingia robo fainali kwa wasichana ni Mara dhidi ya Songwe, Morogoro dhidi ya Katavi,shinyanga itacheza na Tanga na Singida dhidi ya Geita.
Katika mpira wa mikono wavulana, Rukwa itacheza dhidi ya Mwanza, Tabora dhidi ya Morogoro, Pwani dhidi Manyara na Tanga dhidi ya Mbeya.
Robo fainali ya Netiboli itazikutanisha Morogoro dhidi Mwanza, Tanga dhidi ya Songwe, Mara dhidi ya Geita na Dar es salaam dhidi ya Kigoma.
Kwa upande wa matokeo ya riadha mchezo wa kuruka juu Mwanafuni Gani Ngelema kutoka mkoa wa Manyara alitia fora baada kuruka juu umbali wa sentimita 66 na kufuatiwa na Lumnyaki Jacob wa Manyara ambaye aliruka urefu wa sentimita 64.
Kwa wasichana, mwanafunzi Pendo Nila kutoka Simiyu aliruka urefu wa sentimita 36 na kufuatiwa na Aneth John wa Geita ambaye naye aliruka urefu wa sentimita 36