MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Boniphance Luhende,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Mawakili wakifatilia hotuba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo Juni 14,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,amewataka Mawakili wa Serikali nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria ili kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao
Wito huo ameutoa leo Juni 14,2021 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku nne yenye lengo la kuwajengea uwezo Mawakili wa serikali kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Prof.Kilangi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya Sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.
“Mafunzo haya ni kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi na weledi katika utekelezaji wa majukumu yenu na kuboresha mahusiano jambo ambalo ni muhimu katika utendaji kazi, mada muhimu zitagusiwa ikiwamo weledi katika uendeshaji wa mashauri ya madai,”amesema Prof.Kilangi
Prof.Kilangi amesisitiza kuwa mada hizo ni muhimu kwao katika uendeshaji wa mashauri ya serikali ndani na nje ya nchi.
“Lazima muwe na ujuzi wa kusimamia na kuendesha mashauri haya ndani na nje ya nchi inaweza kuwa kwenye Mahakama za Kimataifa au Mabaraza ya kimataifa,”amesema Prof.Kilangi
Pia ameitaka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kushirikiana na Taasisi mbalimbali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ofisi hiyo ikiwemo uhaba wa mawakili wa Serikali.
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata ,amesema ofisi hiyo ilipewa jukumu lakuendesha madai ya kesi ndani na nje ya nchi na kupitia mafunzo hayo yanaenda kuwaweka katika mtazamo mmoja wa uendeshaji wa mashauri kwa niaba ya Serikali na Taasisi zake huku akibainisha mafanikio na changamoto mbalimbali.
Amesema kuwa ofisi hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake mwaka 2018 na kwa kipindi hicho mafanikio mbalimbali yamepatikana ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/20 ofisi hiyo ilifanikiwa kuokoa fedha ambazo zinatokana na mashauri yaliyofunguliwa dhidi ya serikali na taasisi zake Sh.Trilioni 11.4
“Mwaka huo pia ofisi iliendesha mashauri mbalimbali ambayo hayahusishi fedha na kurejesha mali mbalimbali ikiwamo mashamba 106,”amesema Malata