Home Mchanganyiko RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIMSIKILIZA KAIMU MKURUGENZI WA STAMICO ALIPOZINDUA KIWANDA CHA...

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIMSIKILIZA KAIMU MKURUGENZI WA STAMICO ALIPOZINDUA KIWANDA CHA KUCHENJUA MADINI

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Dkt.  Venance Mwasse Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO wakati alipozindua Kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kilichopo Sabasaba mkoani . Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2021, Kwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia na STAMICO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Madini Doto Biteko, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mwanza Antony Dialo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi pamoja na viongozi mbalimbali, akivuta utepe kuzindua Kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kilichopo Sabasaba mkoani Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amezinduwa kiwanda cha kisasa cha kusafisha dhahabu kwa viwango vya kimataifa, (999.9 purity). Uziduzi huo uliyofanyika leo katika maeneo ya kiwanda hicho kilichoko katika Halmashauri ya Manispaa ya ilemela jijini Mwanza. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi Wakuu wa wizara ya Madini Chama na Serikali tukio hili lilirushwa mubashara kupitiaTBC1, Star TV, ITV, Channel Ten, Wasafi TV, Clouds na ETV na tukio hili lilianza saa 3:45 Asubuhi