Wakulima wadogo wa miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwemo kanuni za kilimo bora cha zao hilo, yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania Juni 10, 2021.
Wakulima wadogo wa miwa wakinyoosha mikono kukubaliana kuunda chama cha ushirika.
Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya wakulima wa miwa ambao mashamba yao yamesharasimishwa wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa,Robert Lyanzile aktoa mafunzo kuhusu umuhimu wakulima hao kuanzisha chama chao cha ushirika ili mambo yao yawe yanakwenda vizuri ikiwemo kupata mikopo kwa urahisi.
Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, David Wangere akiendesha mafunzo kuhusu kanuni za kilimo bora cha miwa.
Wakulima wakisikiliza kwa makini wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Afisa Mahusiano Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Kilosa, Joel Danford akielezea umuhimu wa kujiunga na benki hiyo na jinsi ya kupata mikopo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Dumila, Michael Mwabusila akielezea umuhimu wa kuunda vikundi ikiwemo chama cha ushirika.,
Diwani wa Kata ya Dumila, Douglas Mwigumila akioa shukrani kwa uongozi wa Mkurabita kwa kazi nzuri ya urasimishaji mashamba ya wakulima wa miwa katika Kijiji cha Mkundi.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Sandabila akielezea faida za urasimishaji ardhi na jinsi ya kuthaminisha mali.
Na Richard Mwaikenda, Kilosa
Zaidi ya mashamba 263 ya wakulima wadogo wa miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, Morogoro yamerasimishwa kwa lengo la kuyapatia Hati Miliki za Kimila zitakazotumika kuweka dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za kifedha ili kuboresha mashamba yao na miradi mingine.