WENYEJI, England wameanza vyema Fainali za Euro 2020 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi Croatia katika mchezo wa Kundi D jioni ya leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling dakika ya 57 akimalizia pasi ya kiungo wa Leeds United, Kalvin Phillips.